Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil akipiga mpira wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika leo dhidi ya Chelsea katika Uwanja wa Stamford Bridge mjini London. Chelsea imeshinda mabao 3-1. |
LONDON, England
MATUMAINI ya Arsenal ya kushinda taji la Ligi Kuu ya England yameyayuka
baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Chelsea wanaopewa nafasi
kushinda taji hilo.
Kutokana na ushindi huo Chelsea wanaendelea kujikita kileleni mwa msimamo
wa ligi kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya Arsenal yenye pointi 47 na hivyo
kufuta matumaini ya washika ubingwa hao kuwania kushinda taji hilo walilolitwaa
kwa mara ya mwisho mwaka 2004.
Kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Stamford Bridge Chelsea
walitangulia kufunga kwa bao la beki wa kushoto Marcos Alonso kwenye dakika ya
13.
Alonso alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kumzidi nguvu beki wa kulia
wa Arsenal Hector Bellerin aliyeumia katika harakati za kumgombania mpira huo
wa juu na Alonso.
Kutokana na kuumia kwa Bellerin beki wa kimataifa wa Brazil aliingia
badala yake na kupoteza nafasi ya wazi ya kusawazisha kwa kupiga mpira wa
kichwa uliotoka nje ya lango.
Chelsea walifanikiwa kuongeza bao la pili kupitia kwa winga wake Eden
Hazard kwenye dakika ya 53. Hazard alifunga bao hilo kwa juhudi binafsi baada
ya kuwatoka wachezaji wa Arsenal tokea katikati ya uwanja na kupiga shuti
lililompita kipa Petr Cech.
Kiungo wa zamani wa Arsenal Francesc Fabregas dakika za mwisho za mchezo
huo. Fabregas alifunga bao hilo kutokana uzembe wa kipa wa Arsenal wa kupiga
mpira mfupi na kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania kuunasa na kupiga mpira wa
juu uliompita kipa huyo wa zamani wa Chelsea.
Hata hivyo Arsenal walifanikiwa kuambulia kupata bao la kufutia machozi
kwenye dakika ya 90 ya mchezo likifungwa na mshambuliaji wake Olivier Giroud
kwa kichwa.
No comments:
Post a Comment