Na Gilbert Peter
LIGI ya mpira wa kikapu (RBA) mkoa wa Dar es Salaam inataraji kuanza kuchezwa Jumamosi Februari 11 kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, imeelezwa.
Mbali na Uwanja huo wa ndani, mechi za ligi hiyo pia zitachezwa kwenye viwanja vingine vya Gymkhana na Don Bosco- Upanga.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari kwenye
ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, ,Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mmkoa wa Dar es
Salaam (BD), Okare Emesu amesema ligi hiyo
itahusisha timu 16 huku nane zikiwa za wanaume na idadi kama hiyo kwa wanawake.
Alizitaja timu hizo kwa upande wa kiuumeni kuwa ni JKT
,Savio, ABC ,Vijana ,Oilers ,Pazi ,Magereza ,Don Bosco Young
Stars,Mgulani , Magnet ,Jogoo , Chui , Mabibo Bullets ,UDSM Outsiders ,Ukonga Kings na
Kurasini Heat .
Wakati timu za wanawake ni pamoja na JKT ,Jeshi Stars
, Vijana Queens , Don Bosco Lioness , Ukonga Queens,Kurasini Divas
,Oilers Princess na Prisons.
Pia ligi hiyo itakuwa na mfumo wa nyumbani na ugenini katika hatua ya awali na timu nane(8) za wanaume zitakazokuwa nafasi za juu zitacheza hatua ya mtoano (Play Offs) hadi kupata bingwa.
Kwa upande wa kike watacheza mfumo wa ligi, ambapo atakayekuwa wa kwanza ndiye atakayekuwa bingwa wa mchezo huo kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment