Na Mwandishi Wetu
YANGA
imekataa kucheza mchezo wa kujipima
nguvu na mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini Ijumaa,
imeelezwa.
Habari
kutoka Yanga, zimesema kuwa kocha wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina ndiye
aliyegomea mchezo huo akidai kuwa utaingilia program yake ya mazoezi.
Taarifa
zaidi zinadai kuwa, Lwandamina amekataa mchezo dhidi ya Mamelodi uliokuwa ufanyike
Ijumaa kwa madai kuwa unaingilia mipango yake.
“Hatutacheza na Mamelodi kwa sababu kocha
ameukataa huo mchezo, amesema unaingilia programu zake, kama unavyojua kwa sasa
tupo kwenye hatua ngumu ya Ligi Kuu na wakati huo huo tunaingia kwenye Ligi ya
Mabingwa Afrika,”kilisema chanzo chetu.
Baada
ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui FC, Yanga SC itamenyana na timu nyingine ya
Shinyanga ya Stand United Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika
mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa
upande wake, waandaaji wa mechi hiyo pamoja na kusikitishwa na kitendo cha
Yanga kugomea mchezo huo, lakini tayari wameiteua Azam FC kuchukua nafasi hiyo.
Sasa
Memelodi baada ya kucheza na Simba kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam, watahamia Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam Ijumaa kucheza na Azam.
Timu
hiyo inakuja nchini kwa mwaliko wa klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa African Lyon, Rahim Kangenzi ‘Zamuda’ alisema Mamelodi wanakuja nchini
kushiriki kampeni ya kupiga vita ujangili, iitwayo Linda Tembo Wetu.
Na
Zamunda amesema timu hiyo ya mjini
Pretoria itakuwa nchini kwa wiki yote ya kwanza Februari kushiriki kampeni hiyo
pamoja na kucheza mechi hizo.
Kuhusu
kujiondoa kwa Yanga, Zamunda alisema kwamba hawana cha kufanya zaidi ya
kukubaliana nao, lakini amesikitishwa na hilo.
No comments:
Post a Comment