MANCHESTER, England
MANCHESTER City haina mpango wa kumuuza Sergio Aguero katika kipindi hiki
cha Majira ya Joto, licha ya mshambuliaji huyo kutopangwa katika mechi mbili zilizopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alisaini kuongeza mkataba mapema
mwaka huu, ikiwa na maana kuwa amebakiza miaka mitatu kabla ya kumaliza mkataba
huo.
Baada ya kuingia akitokea benchi wakati Man City ikishinda mabao 2-1
dhidi ya Swansea, Aguero alisema: "Bila shaka nataka kuendelea kubaki
hapa.
"Katika miezi hii mitatu natakiwa kuisaidia klabu na wao ndio watakaoamua
hatma yangu kama nitaendelea kuhitajika hapa au la.”
Kipa wa Manchester City, Willy Caballero akishangilia.
|
Licha ya Aguero kutarajia uamuzi kufanywa wakati wa kipindi cha majira ya
joto, mmoja wa wazito katika klabu ya Man City alidokeza juzi kuwa hawana
mpango wa kumuuza mchezaji huyo.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliingia akitokea benchi
wakati Man Cuty ikiibuka na ushindi mzuri dhidi ya Swansea shukrani kwa bao la
ushindi la dakika za mwisho la Gabriel Jesus, la mchezo wa pili wa Mbrazil
huyo, aliyechukua nafasi ya Aguero katika kikosi cha kwanza.
Aguero ndiye mfungaji anayeongoza kwa kufungamabao mengi Man City, ambapo
msimu huu amefunga mabao 18, ikiwa 11 zaidi ya Raheem Sterling, ambaye
anafuatia katika orodha hiyo.
Ni mchezaji wa tatu kufunga mabao mengi katika kipindi chote Man City
akiwa na mabao 154 na alikuwa mshindi wa kiatu cha dhahabu katika Ligi Kuu
katika msimu wa mwaka 2014-15.
Pia ndiye mfungaji anayeongoza kwa kupachika mabao katika msimu wa mwaka
2011-12 katika kampeni zake za kutwaa ubingwa.
No comments:
Post a Comment