Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon wakishangilia bao lao la pili walipocheza nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (afcon) dhidi ya Ghana. Cameroon ilishinda mabao 2-0. |
LIBRAVILLE, Gabon
FAINALI ya Kombe la Mataifa Afrika, AFCON, itachezwa kesho, ambapo timu
ya Cameroon itaumana na Misri huku Ghana ikiwa imekosa kwa mara nyingine
kucheza fainali hizo.
Katika mchezo wa Cameroon na Ghana timu zote zilicheza kwa kiwango kizuri
huku kila mmoja akijitaidi kufanya vema, ambapo Cameroon ilionekana kutumia
vema nafasi ilizozipata na kuibuka na ushindi wa 2-0.
Mchezaji wa Cameroon, Michael Ngadeu-Ngadjui mnamo dakika ya 72
aliandikia bao la kwanza timu yake hiyo huku mwenzake Christian Bassogog
akiandika bao la ushindi zikiwa zimebakia dakika za mwisho mchezo kumalizika.
Ghana kwa upande wake kupitia wachezaji wake akina Wakaso Mubarak na
Christian Atsu iliendelea kusaka mabao bila ya mafanikio.
Wakaso anaechezea timu ya Panathinaikos
nafasi ya kiungo aliachia shuti kali kuelekea lango la Cameroon lakini
liliondolewa na kipa Fabrice Ondoa, mwenzake Atsu saw anaechezea New Castle
alipiga shuti lakini lilipita juu la lango la Cameroon.
Ghana iliibuka na ubingwa wa kombe hilo mwaka 1982 huku Cameroon ikiwa
imecheza na kufikia hatua za juu pia kwenye michuano hiyo.
Kwa upande wake kocha wa Cameroon, Hugo Broos amesema kuwa ni sawa na
ndoo iliyokuja kuwa kweli ka timu yake kufikia hatua hiyo ambapo mara ya kwanza
kucheza fainali tangia mwaka 2008 ilipopoteza dhidi ya Misri.
Alisema kuwa timu kama ya Ghana ina uzoefu na michuano mbalimbali mikubwa
lakini kwa timu yake imeweza kufanya tangia kuanza kwa michuano hiyo.
Alisema"ninakipenda kikosi changu na kuwa nina imani nacho sana kwa
kuwa wachezaji wangu wamekuwa wakicheza kwa amani na uwezo wa hali ya juu kila
wakati".
Alisema kuwa wachezaji wake walicheza licha ya kuwa timu shindani, Ghana,
ilikuwa na wachezaji wakubwa kama akina Andre Ayew na kaka yake Jordan pamoja
na Asamoah Gyan.
Beki wa Cameroon Ngadeu-Ngadjui ambae anachezea timu ya Slavia Prague
alionesha umahiri mkubwa kwenye safu ya ulinzi huku akiisaidia kupata bao la
kwanza kwa itmu yake hiyo.
Aliachia shuti kali lililomwacha beki wa Ghana John Boye na kipa wake
Razah Brimah wasijue la kufanya.
No comments:
Post a Comment