CAIRO, Misri
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limeirejesha
Tanzania kushiriki katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kushinda rufaa yake.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimkatia rufaa mchezaji wa Congo
Brazzaville, Langa-Lesse Bercy aliyechezeshwa baada ya kuzidi umri.
Katika mchezo wa mwisho kabla ya kufuzu, Serengeti Boys ilishinda bao 3-2
jijini Dar es Salaam kabla ya kufungwa 1-0 na kutolewa kwa faida ya bao la
ugenini.
TFF ilikata rufaa kupiga kuchezeshwa kwa mchezo huyo, ambapo Caf iliamuru
afanyiwe vipimo vya kugundua umri wake halisi,
lakini mara kadhaa mchezaji huyo hakutokea.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye jana
alikaririwa na Radio ya TBC Taifa, ambapo alithibitisha kuwa, Tanzania
imeshinda rufaa yake na sasa itashiriki fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa
vijana yatakayofanyika baadae mwaka huu.
Serengeti Boys inaendelea na maandalizi ya mashindano katika hostelini za
TFF zilizopo Karume tayari kushiriki mashindano.
Tanzania iliondolewa kushiriki katika fainali za mwaka 2005 zilizofanyika
Gambia baada ya kumchezesha Nurdin Bakari aliyezidi umri.
No comments:
Post a Comment