Na Gilbert Peter
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Kamati ya Olimpiki
Tanzania, Irene Mwasanga ameshinda ukatibu mkuu wa Chama cha Mpira wa Tenisi Tanzania (TTA).
Katika uchaguzi huo mkuu uliofanyika jana kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mwasanga ambaye pia ni mwenyekiti wa
Kamati ya Wanawake ya Kamati ya Olimpiki za Afrika, aipata kura 15 za ndio.
Rais wa mpya wa TTA ni Dennis Sirito Makoi aliyepata
kura za ndio 16 wakati makamu wake ni John Bura aliyepata kura 16.
Walioshinda katika nafasi ya ujumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TTA, ni pamoja na Mosses Mabula aliyepata kura 13, Rehema Mbegu
aliyepata kura 16, Rizik Salum Seleman kura 15.
Wengine walioshinda nafasi hizo za ujube wa Kamati ya
Utendaji ni pamoja na Sanjay Choksh alipata kura 13.
Uchaguzi huo uliosimamiwa na Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) umefanyika baada ya TTA kutokuwa na viongozi kwa muda baada ya
baadhi ya kuachia ngazi kwa sababu tofauti.
Aidha, viongozi hao wapya wana kibarua kizito kuhakikisha wanalipa madeni kibao yaliyoachwa na uongozi uliopita pamoja na kuuendeleza mchezo huo.
Aidha, viongozi hao wapya wana kibarua kizito kuhakikisha wanalipa madeni kibao yaliyoachwa na uongozi uliopita pamoja na kuuendeleza mchezo huo.
No comments:
Post a Comment