Na Mwandishi Wetu
SIMBA leo ina nafasi ya kuiengua Yanga kileleni katika msimamo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara, endapo itaifunga Tanzania Prisons katika mchezo
utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wekundu hao wa Msimbazi wanahitaji ushindi kwa nguvu kwani lengo lao sio
tu kuwaondoa watani zao kileleni, bali pia wanataka kulipa kisasi cha kufungwa
na Prisons katika mzunguko wa kwanza katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine.
Simba wako katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga wakiwa na pointi 48 na
kama wakishinda leo watafikisha 51 na kurejea katika kilele cha msimamo wa ligi
hiyo inayoshirikisha timu 16.
Yanga wenyewe leo hawatashuka dimbani kwani wako `angani’ wakienda Comoro
kucheza na mabingwa wa huko Ngaya De Mbe katika mchezo utakaofanyika kesho
Jumapili.
Kutoshuka uwanjani kwa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
kunaipa mwanya Simba kushika usukani endapo wakishinda watafikisha pointi 49 na
kuifikia Yanga.
Yanga watakuwa na mchezo mmoja pungufu, huku Simba baada ya mchezo wa leo
itakuwa imefikisha mechi 22 na kubakisha nane kabla ya kufungwa kwa mbio hizo
za ubingwa.
Ushindi wa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo umeongezeka mara dufu hasa baada
ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kuwa mshindi wa kwanza ndiye
atawakilisha taifa katika Ligi ya Mabingwa huku mshindi wa pili akitoka kapa.
Hatahivyo, Simba wasitarajie mteremko kwani Prisons wako vizuri na
wanaingia uwanjani huku wakiwa wameshinda mechi mbili mfulululizo
zilizotangulia,,kitu ambacho kinawafanya wawe na ari kubwa.
Prisons ilipata ushindi dhidi ya maasimu wao Mbeya City kwa mabao 2-0
kabla ya kuifunga 2-1 Ruvu Shooting na kuzidi kuwa na ari ya ushindi bila
kujali timu itakayocheza nayo.
Mshindi wa Kombe la Mashindano ya Kombe la FA ndiye atakayeliwakilisha
taifa katika mashindano ya Shirikisho la Afrika, hivyo kubakisha nafasi moja tu ya mshindi wa Ligi Kuu kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Afrika, wakati huko nyuma mshindi wa pili wa Ligi Kuu alikuwa akishiriki Kombe la Shirikisho.
Mechi zingine za leo ni kati ya Azam FC itakayocheza dhidi ya Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi, huku Stand United ikiikaribisha
Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Toto Africans ya Mwanza ikaikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba wakati kesho African Lyon itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar na Mwadui ya
Shinyanga watawakaribisha Mbeya City.
Msimamo:
MP
|
W
|
D
|
L
|
G
|
P
|
||
1
|
Young
Africans
|
21
|
15
|
4
|
2
|
+37
|
49
|
2
|
Simba
|
21
|
15
|
3
|
3
|
+26
|
48
|
3
|
Azam
|
21
|
10
|
7
|
4
|
+10
|
37
|
4
|
Kagera
Sugar
|
21
|
11
|
4
|
6
|
+4
|
37
|
5
|
Mtibwa
Sugar
|
21
|
8
|
7
|
6
|
-2
|
31
|
6
|
Tanzania
Prisons
|
22
|
7
|
8
|
7
|
-1
|
29
|
7
|
Ruvu
Shooting
|
21
|
6
|
9
|
6
|
-3
|
27
|
8
|
Mbao
|
21
|
7
|
5
|
9
|
+0
|
26
|
9
|
Stand
United
|
21
|
6
|
8
|
7
|
-2
|
26
|
10
|
Mbeya
City
|
21
|
6
|
8
|
7
|
-2
|
26
|
11
|
Mwadui
|
21
|
7
|
4
|
10
|
-9
|
25
|
12
|
African
Lyon
|
21
|
4
|
10
|
7
|
-6
|
22
|
13
|
Ndanda
|
21
|
5
|
5
|
11
|
-14
|
20
|
14
|
Toto
Africans
|
21
|
4
|
6
|
11
|
-10
|
18
|
15
|
Maji
Maji
|
21
|
5
|
3
|
13
|
-17
|
18
|
16
|
Ruvu
Stars
|
22
|
2
|
11
|
9
|
-11
|
17
|
No comments:
Post a Comment