Saturday 11 February 2017

mashabiki wa soka 17 wauawa katika vurugu za soka uwanjani Angola



LUANDA Angola
ANGALAU watu 17 wameuawa baada ya kukanyagana kwenye Uwanja wa Soka kaskazini ya mji wa Angola wa Uige, imeelezwa.

Mamia ya mashabiki waliripotiwa kuumia walipovunja geti baada ya kutaka kuingia uwanjani kwa nguvu baada ya kuzuia.

Baadhi yao walianguka na kukanyagwa na kukosa hewa kwenye uwanja huo Ijumaa, viongozi wa madaktari walieleza,

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema watu walijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza watazamani 8,000 tu.

Santa Rita de Cassia ilikuwa ikicheza na Recreativo do Libolo katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza.

"Baadhi ya watu ilibidi kuwakanyaga wengine. Kuliuwa na majeruhi 76, ambao kati yao 17 walikufa,”alisema Ernesto Luis, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo.

Watu watano iliripotiwa kuumia vibaya katika tukio hilo.

Vyombo vya habari vya vya Angola na Ureno viliripoti kuwa, baadhi ya waliokufa ni watoto.
Katika taarifa ya klabu ya Recreativo de Libolo uliliita tukio hilo kuwa ni "janga la kwanza kutokea katika hostoria ya soka la Angola”.

Shabiki wa soka Domingos Vika, 35, alisema kuwa mlango wa kuingilia tayari ulikuwa umefurika wakato watu zaidi wakimiminika uwanjani.

"Wakati kila mmoja alipopewa nafasi ya kuingia, wote tulijazana katika geti, “alisema Vika, aliyeondoka uwanjani huko akiwa amrvunjika mkono.

Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos ameagiza ufanyike uchunguzi kuhusu tukio hilo, vimeripoti vyombo vya habari.

Mchezo huo ulimalizika kwa usindi wa bao 1-0 kwa timu ya nyumbani kufungwa, ambayo ni Santa Rita de Cassia.

No comments:

Post a Comment