Friday, 3 February 2017

Kocha ghana asikitikia kufungwa na Cameroon, akisifu kikosi chake cha Afcon 2017



LIBRAVILLE, Gabon
AVRAM Grant hawezi kuficha huzuni yake baada ya Ghana (pichani) kufungwa mabao 2-0 na Cameroon katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika juzi, lakini anasisitiza kuwa mashindano yalikuwa mazuri kwa Black Stars.

Hiyo ilikuwa mara ya sita kwa Ghana kucheza nusu fainali ,lakini waliondolewa kwa mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Michael Ngadeu na Christian Bassogog huko Franceville na bado hawajawahi kushinda taji hilo tangu mwaka 1982.

"Nafikiri hadi hapa tulipodikia tumepata mafanikio makubwa,”alisema Grant alipoulizwa Ghana ilivyoshindwa kusonga mbele katika mashindano hayo hivi karibuni.

"Hatujashinda taji lakini tulikuwa na wakati mzuri katika mashindano haya. Leo tulikuwa timu nzuri, na katika mashindano ya mwisho tulishindwa kwa penalty.”

Miaka miwili iliyopita Ghana ilicheza fainali ya michuano hiyo iliyofanyikia Equatorial Guinea na ilifungwa na 9-8 kwenye mikwaju ya penati na Ivory Coast.

Kocha huyo alisema kuwa anaiona timu hiyo kuwa ni nzuri na ni kizazi kipya na wanaweza kuja kushinda makombe  mengi makubwa kwa baadae.

Ghana bado inaweza kufuzu kucheza mchuano ijayo ya Kombe la Dunia itakayofanyika Urusi ambapo ilianza harakati zake hizo Congo Brazzaville, Agost mwaka jana lakini bado inangojewa kama bado kocha Grant ndio ataendelea kuinoa timu hiyo.

Kocha huyo raia wa Israel ambaye aliwahi kuwa kocha wa Chelsea alisema kuwa kwa sasa hataki kuzungumzia kuhusiana na suala zima la maisha yake ya soka, ila ni kuonesha masikitiko yake ya kutolewa kwenye michuano hiyo muhimu kwenye hatua ya nusu fainali.

Timu hiyo imerejea kwenye eneo la Port-Gentil,  ambapo walicheza kwenye hatua ya makundi ili kujipanga kucheza dhidi ya Burkina Faso kuwania nafasi ya tatu, mchezo utakaochezwa leo.

No comments:

Post a Comment