Na Mwandishi Wetu
TIMU tano zimefuzu hatua ya sita bora ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara
baada ya hatua ya makundi, wakati mechi za mwisho zitaamua timu ya mwisho ya
kukamilisha hatua hiyo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ameiambia
leo Bin Zubeiry Sports – Online kwamba kutoka Kundi B timu zote tatu za kusonga
sita bora zimekamiliaa mbazo ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya
Pwani na Fair Play ya Tanga.
Timu zilizikosa nafasi ya kusonga mbele kutoka kundi hilo ni Evegreen ya
Temeke, Mburahati Queens ya Dar es Salaam na Viva ya Mtwara.Lucas alisema timu
zilizofuzu hadi sasa kutoka Kundi A ni Sisters ya Kigoma na Marsh Academy ya
Mwanza.
Timu nyingine zilizobaki ambazo zinawania nafasi moja ya kukamilisha
timu za kufuzu Sita Bora kutoka kundi hilo ni Panama ya Iringa, Baobab ya
Dodoma, Majengo ya Singida na Victoria na Queens ya Kagera.
Hatua ya Sita Bora inatarajiwa kuanza katikati ya mwezi Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam na bingwa atajainyakulia Kombe na Medali za rangi ya Dhahabu,
mshindi wa pili Kombe na Medali za rangi ya Fedha.
No comments:
Post a Comment