Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeitaka timu ya Tanzania
itakayoshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki kuhakikisha inarejea na medali kutoka
katika michezo hiyo nchini Brazil.
Michezo hiyo itaanza Ijumaa hadi Agosti 21,
ambapo timu hiyo yenye wachezaji wa riadha (4), kuogelea (2) na judo (1),
iliagwa jana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia
Wambura kwenye Uwanja wa Taifa.
Wabura katika hafla hiyo alisema kuwa
anatambua changamoto kibao walizopitia wanamichezo hao wakati wa maandalizi ya
kushiriki michezo hiyo mikubwa inayoshirikisha zaidi ya mchezo mmoja duniani.
Pia, naibu waziri huyo aliwapongeza
wanamichezo wote waliofuzu na wale wanaoshiriki michezo hiyo kwa upndeleo kwa
jitihada zao walizofanya wakati wakijiandaa kwa michezo hiyo.
Aliwataka wachezaji hao kupambana ili
kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania na kutangaza utamaduni wa Tanzania
zikiwemo ngoma za asili.
Pia aliwapongeza wadhamini mbalimbali, ambapo
aliwataka kudhamini na michezo mingine ambayo haipewi kipaumbele.
Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa
Elisante Ole Gabriel aliwataka Bodi ya Utalii (TTB) kuwapeleka wanamichezo hao
katika mbuga za wanyama watakaporejea kutoka Brazil.
Wanariadha wanaounda timu hiyo ni Alphonce
Felix, Said Makula, Fabian Joseph na mwanadada pekee katika riadha, Sarah
Ramadhani, ambao wote watashiriki marathon.
Waogeleaji ni Magdalena Moshi na Hilal Hemed
Hilal wakati mchezaji pekee wa judo ni Andrew Thomas.
Makocha watakaoongozana na timu hizo ni
Francis John (riadha), Alexander Mwaipasi (kuogelea) na Zaid Hamisi (judo)
wakati daktari wa timu ni Nassoro Matuzya.
Waogeleaji na mchezaji huyo wa judo na
makocha wao wanaoondoka leo kwa ndege mbili tofauti, huku mwanariadha wakike
ataondoka Agosti 10 na wale wakiume wataondoka Agosti 15.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizunggumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla. |
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC), Filbert Bayi alisema timu hiyo inaondoka kwa awamu kutokana na ratiba za
ndege.
Timu ya judo itaondoka kwa ndege ya Afrika
Kusini na kundi la pili litakuwa la kuogelea, ambalo litaondoka saa tisa
alasiri na Emirates.
Mkurugenzi Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuiaga timu ya Tanzania ya Olimpiki kwenye Uwanja wa Taifa. |
Nahodha wa timu hiyo, Felix alisema timu ya
riadha imejioandaa vizuri baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, ambapo
aliahidi kurudi na medali.
Jenerali Mstaafu Mrisho Sarakikya (kushoto) akiwa na kiongozi wa mpira wa meza na mjumbe wa TOC. |
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya Olimpiki wakichukua msosi walipoandaliwa chakula cha mchana katika hoteli ya Lamada. |
Wachezaji wa timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya Olimpiki wakipata mlo katika hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam. |
Medali huwa zinatabirika hasa ktk riadha kwa sababu mshindi ni yule aliyemaliza ndani ya MUDA MFUPI. Mchezaji makini anajijua huwa anamaliza mbio za mita elf 10 kwa dakika ngapi. Halafu analinganisha na rikodi ya dunia au ya olimpiki iliyopita. Kwa hiyo wachezaji na viongozi TAYARI wanajua km medalist IPO AMANI HALIPO.
ReplyDelete