LONDON, England
KIUNGO wa Arsenal Jack Wilshere ameambiwa na kocha Arsene Wenger kuwa
atakuwa huru kuondoka katika klabu hiyo ya Ligi Kuu kabla ya kunaza kwa msimu,
lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameamua kupigania namba.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akipigania nafasi
ya kuanza katika klabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni baada ya kusumbuliwa
na maumivu na alitumia kampeni akicheza kwa mkopo Bournemouth kabla hajaumia
mguu Aprili mwaka jana.
Wilshere aliambiwa kuwa anamweza kuondoka wakati ukiwa umebaki
mwezi mmoja katika kipindi cha usajili cha majira ya joto lakini hakuna ofa
zakutosha kutoka klabu zingine, kitu ambacho kinamfanya kupigania kuwa fiti
kwanza.
"Yalikuwa maongezi mazuri, “alisema Wilshere alipozungumza na
vyombo vya habari vya Uingereza. "Yeye (Wenger) alisema, nitakuwa
mwaminifu na wewe na kwa sasa sitakupatia mkataba, hivyo kama utapata mkataba
mahali kwingine, unaweza kwenda tu'.
"Ni wazi, Sina furaha na hilo lakini wakati huo huo nilikuwa
na furaha….
"Pia alisema kuwa kama nitaendelea kubaki nitakuwa na nafasi
ya kupambana ili kupata namba katika kikosi cha kwanza, na nilicheza vizuri
katika Kombe la Ligi na Ligi ya Ulaya. Nina nafasi bao.”
Wilshere amekuwa akipambana kuwania nafasi katika kikosi cha
kwanza, akicheza mechi 31 katika klabu hiyo msimu huu na aliitwa katika kikosi
cha England kwa mara ya kwanza mwaka 2016.
Kiungo huyo mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu na Wilshere
anataka kuhakikisha anapambana ili kurejesha kiwango chake kabla ya kuanza kwa
Kombe la Dunia Juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment