Saturday, 17 March 2018

Nyota Bollywood Kushuhudia Tuzo za Sinema Zetu

Na Mwandishi Wetu
MSANII maarufu wa tamthilia ya Kihindi ya Beintehaa, Preetika Rao au maarufu kwa jina la Aliyah atakuwa mgeni maalum katika hafla ya utoaji tuzo za Sinema Zetu utakaofanyika Aprili Mosi.

Aliyah ambaye anajulikana sana na watumiaji wa kingamuzi cha Azam, ambacho kilikuwa kikirusha tathilia ya Beintehaa kila kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 3:30 usiku.
Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando alisema jana kuwa, Alia atakuwa mgeni maalum wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo utakaofanyika katika ukumbi wa Mlima City jijini Dar es Salaam.

Azam TV kupitia chaneli yake ya sinema zetu imetangaza vipengele 18 vya filamu zitakazowania tuzo za Sinema Zetu International Film Festival ikiwemi kipengele cha chaguo la watazamaji.

Mhando alisema kuwa Usiku wa Tuzo za SIFF utaruka moja kwa moja kutoka Mlimani City kupitia chaneli ya Sinema Zetu, ambapo wageni waalikwa watapita katika zuria jekundu.

Baadhi ya vipengele ambavyo vinagombewa ni pamoja na Filamu Bora, Muongozaji Bora, Muigizaji Bora, Mchekeshaji bora.

Huku katika kipengele cha filamu fupi kuna tuzo ya filamu bora, muongozaji bora, muziki bora na mambo mengine.

Tido alisema kuwa mbali na Aliyah kutakuwa na watu wengine maarufu pamoja na mgeni rasmi, ambaye atatajwa baadae.

Jumla ya filamu 143 zilipata nafasi ya kupambanishwa na kuruka kila siku kupitia chanel ya Sinema Zetu, ambapo watazamaji walipata nafasi ya kupiga kura kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno.

No comments:

Post a Comment