LONDON, England
KLABU Southampton
imemtupia virago kocha wake Mauricio Pellegrino (pichani) huku timu hiyo ikiwa pointi
moja na nafasi moja juu ya ukanda wa kushushwa daraja wakati zimebaki mechi
nane kabla ya kumalizika kwa msimu.
Watakatifu hao
wameshinda mechi moja tu kati ya 17 za ligi zilizopita na ilifungwa mabao 3-0
huko Newcastle United Jumamosi.
Pellegrino, mwenye
umri wa miaka 46, aliteuliwa kuifundisha timu hiyo Juni akichukua nafasi ya Claude
Puel.
Timu hiyo ina
matumaini ya kuwa na kocha mpya kabla haijakabiliana na Wigan Jumapili kwa
ajili ya kusaka nafasi ya nusu fainali ya Kombe la FA.
Wako katika msimu
wa sita mfululizo katika Ligi Kuu ya England na hawajawahi kumaliza chini ya
nafasi ya 14 katika misimu mitno iliyopita.
Pellegrino alisema
ameona baadhi ya wachezaji waliokatatamaa wakati wa mchezo wa Jumamosi.
Pellegrino, mcheszaji
wazamani wa kimataifa wa Argentina, alipata pointi 0.93 kwa mchezo, ikiwa ni
asilimia mbaya zaidi kwa kocha yeyote wa Southampton katika Ligi Kuu.
Klabu hiyo
ilisema katika taarifa yake kuwa wanataka kuteua timu mpya ya uongozi haraka
iwezekanavyo, tayari hilo liko katika mchakato.
Ni timu ya tisa
ya Ligi Kuu kubadili kocha msimu huu.
Kocha msaidizi Carlos
Compagnucci na kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza Xavier Tamarit nao pia
wameondoka katika klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment