Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa kwanza wa mbio za Heart Marathon ambazo sasa
zitafanyika Aprili 29 badala ya Aprili 26, atazawadiwa kiasi cha Sh milioni 2.
Akizungumza na waandishi wa habari Mikocheni, Dar es Salaam jana, Katibu
Mkuu wa mbio hizo, Rebecca John alisema kuwa, wamebadilisha tarehe ya kufanyika
mbio hizo baada ya kuombwa na wadau.
John alisema kuwa lengo kuu la mbio hizo ni kuhamasisha mfumo bora
wa maisha unaosaidia kupunguza kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza kama magonjwa
ya moyo, kisukari, presha na saratani.
Mbali na mbio za kilometa 21, Heart Marathon pia inashirikisha
mbio za baiskeli za umbali huo, zile za meta 700 kwa watoto wenye umri chini ya
miaka 12, kimoeta 10 na zile za kilometa tano,
Akitangaza zawadi kwa washindi kuwa mshindi wa kilometa 21 kwa
upande wa wanawake na wanaume, kila mmoja ataondoka na Sh 2 wakati mshindi wa
pili Sh milioni 1.5 na yule watatu atapewa Sh milioni 1.
Alisema kuwa zawadi zimeongezwa sana, ambapo katika mbio za mwaka
huu mshindi wan ne hadi wa 10, kila mmoja atapewa kifuta jasho cha Sh 100,000
tofauti na miaka ya nyuma, ambapo washindi watatu tu ndio waliokuwa wakipewa
zawadi hizo za fedha.
Mbali na kutoa zawadi kwa watakaokuwepo katika 10 bora, pia
waandaaji wameongeza zawadi kwa washindi kutoka Sh 500,000 ya mwaka jana hadi
milioni 2 za mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, Lukas Nkungu akizungumza na waandishi kuhusu mbio za Heart Marathon leo Mikocheni, Dar es Salaam. |
Mwakilishi wa Riadha Tanzania, Tullo Chambo alisema kuwa wako tayari kuwasaidia waandaaji wa mbio hizo ili kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kuuendeleza mchezo huo nchini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Lukas Nkungu alisema kuwa wako pamoja na waandaaji hao, ambapo aliwaomba watu kujitokeza kwa wingi ili kupima afya zao baada ya kushiriki mbio hizo siku hiyo
No comments:
Post a Comment