MOSCOW, Urusi
MOTO mkubwa ulioua watu 64, wakiwemo watoto 41, katika kumbi za
burudani nchini Urusi, ulisababishwa na `uzembe’, amesema Rais Vladimir Putin.
Putin aliyasema hayo wakati alipotembelea eneo la tukio huko Kemerovo,
Siberia.
Wachunguzi walisema kuwa alamu za moto zilizimwa kwa makusudi, huku
milango ya kutokea nje ikifungwa wakati moto huo ulipoanza juzi Jumapili.
Shirika la Habari la Interfax liliripoti kuwa watu kama 300
walikuwa wamejazana nje ya makamu makuu ya serikali ya mitaa wakitaka
kuondolewa kwa viongozi wa mamlaka hiyo.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, lakini Kamati ya
Uchunguzi imesema kuwa kulikuwa na uvunjifu mkubwa wa taratibu katika duka hilo kubwa la Winter
Cherry mall.
"Nini kilichotokea hapa?",alisema Rais wa Urusi baada ya
kuweka shada la maua katika eneo hilo la tukio.
"Watu, watoto walikuja kupumzika, lakini sasa tunazungumzia
janga. Tumewapoteza watu wengi kwa sababu gani?...”
Jumapili ilikuwa siku ya mapumziko na watoto wengi walifika hapo na
kucheza juu ghorofani bila ya kuwa chini ya uangalizi ya watu wazima, ambao
kama wangekuwepo wangeweza kuwasaidia.
Irina alisema katika gho;ofaya pili watu walianza kupiga keleke “Moto
moto”. Nilijaribu kurudi nyuma, lakini njia yangu ilizuiwa, watu walikuwa wengi.”
Wazazi wa mtoto aliyekuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa
alifanikiwa kuokolewa na marafiki zake. Darina aliungana tena na wenzake katika
ghorofa ya kwanza.
Jumba hilo ambalo lilifunguliwa mwaka 2013, lina kumbi nyingi za
sinema, migahawa na vituo kadhaa vya bafu za maji ya mvuko.
Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari
ya kuporomoka.
Moto huo ulianza katika ghorofa ya juu katika jumba Winter Cherry.
Inadaiwa wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema.
No comments:
Post a Comment