PARIS, Ufaransa
CHIPUKIZI
mshambuliaji wa Paris Saint-Germain (PSG) Tim Weah, mtoto wa Rais wa Libelia na
mchezaji bora wa dunia wa mwaka 1995 George Weah, ndiye mchezaji ndogo zai
kuitwa katika kikosi hicho kwa ajili ya mchezo dhidi ya Paraguay.
Kocha wa muda wa
timu ya taifa ya Marekani Dave Sarachan alitangaza orodha ya wachezaji kwa
ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki Machi 27 itakayofanyika Cary,
Kaskazini
ya Carolina, ambayo itashirikisha wachezaji 17 kati ya 22 wenye umri wa miaka
24 au chini ya hapo.
Weah, 18, anajiunga
kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo ya timu ya taifa ya Marekani baada ya kukichezea
mara mbili kikosi cha kwanza cha PSG wakati ikishinda 2-0 huko Troyes na ule wa
5-0 dhidi ya Metz.
Wamarekani
wameamua kumuinua mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 23 na siku 84 kwa ajili ya kukutana na nchi hizo, ambazo
zimeshindwa kufuzu kwa Kombela Dunia Juni nchini Urusi.
"Mchezo huu
kwa mara nyingine tena inawakilishwa na baadhi ya sura mpya, “alisema Sarachan. "Sehemu kubwa ya
kundi hili ni wachezaji vijana ambao tunafikiri watakuwa na muda mrefu na timu
hiyo ya taifa pamoja na wachezaji wengine wazoefu.”
Weah ni mmoja
kati ya wachezaji watano walioitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha
Marekani, pia kinamjumuisha mabeki Antonee Robinson wa Bolton Wanderers, Erik
Palmer-Brown wa Ubelgiji.
Wengine ni Bortrijk
wa Ubelgiji na Shaq Moore anayeichezea klabu ya Hispania ya Levante pamoja na
mshambuliaji Andrija Novakovich wa timu ya Uholanzi ya Telstar.
"Huu ndio
muda sasa kuwapatia hawa vijana uzoefu wa mechi za kimataifa, “alisema Sarachan. “Watapimwa dhidi ya timu yenye uzoefu ya Paraguay."
Palmer-Brown hivi
karibuni lisajiliwa na vinara wa Ligi Kuu ya England ya Manchester City na yuko
kwa mkopo katika klabu ya Ubelgiji, ambako alianza kuichezea wiki mbili
zilizopita.
Mzaliwa wa
Uingereza Robinson ameichezea mara 29 timu ya Daraja la Kwanza ya Bolton.
No comments:
Post a Comment