Saturday, 17 March 2018

Azam Yatangaza Filamu Zinazowania Tuzo ya SZIFF


Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tuzo za SZIFF. Kushoto ni Mkurugenzi Mratibu wa Vipindi wa Uhai Production, Yahaya Mohamed Kimaro.
Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa Tuzo za Sinema Zetu International Festival (SZIFF), Azam TV wametangaza sinema ambazo zitashindania aina 19 ya tuzo, ambazo zitatolewa Aprili mosi katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kutangaza rasmi sinema zikakazowania tuzo hiyo, Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando alisema wameamua kuandaa tuzo hizo za kila mwaka ili kuwatia moyo wasanii wa Bongo Movie.
Jaji Mkuu wa SZIFF, Martin Mhando akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Msimamizi wa Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi waAzam Media Ltd, Jacob Joseph
Alisema tuzo hizo zinafanyika kwa mara ya kwanza zitasaidia pia kuwawezesha wasanii wa filamu Tanzania kuboresha kazi zao, kutafuta soko ndani nje ya nchi.

Mhando alisema kuwa tuzo za SZIFF ambazo pia zinahusisha wasanii kutoka Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wenyeji Tanzania zitasaidia kurejesha heshima iliyopotea ya Bongo Movie.

WASANII MAARUFU
Mhando alisema kuwa hafla hiyo, mbali na kuwaleta pamoja wasanii maarufu duniani,pia kutakuwa na mgeni maalum kutoka Bollywood ya India Pritika Rao au maarufu kama Aliyah.
Mkurugenzi Msaidizi wa Azam Media Ltd, Jacob Joseph akizungumza. Kulia ni Jaji Mkuu wa SZIFF, Martin Mhando.
Alisema kuwa msanii huyo nyota wa Bollywood alikuwa kivutio cha watazamaji wengi wa filamu nchini kupitia Azam TV kupitia tamthilia ya Beitehaa.

Washindi wa tuzo kwa mujibu wa waandaaji kupitia chaneli ya Sinema zetu, watapata fedha taslimu, vyeti na zawadi zingine kama vikombe maalum.
Msimamizi wa Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mhando alisema tuzo za SZIFF ambazo zinaandaliwa kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bodi ya Filamu na Cosota zilianza Januari na kumalizika Machi 12.

“Tulipokea zaidi ya filamu 500 na vilichujwa hadi kufikia 143 ambazo sasa zinawania tuzo hizo 19, alisema Mhando katika mkutano huo na waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa jop[o la majaji Martin Mhando, alitangaza sinema ambazo zinawania tuzo hizo 19, zikiwemo Chaguo la Watazamaji, ambazo kwa upande wa Filamu Bora ni Bantu, Genge, Safari ya Gwalu, Watatu, The Dream, Heaven Sent, Bandidu, Harusi ya
Teja na Haki ya Nani.
Filamu ambazo ziwania tuzo ya muongozaji bora ni Bantu, Chaguo Langu, Safari ya Gwalu, Watatu, The Dream, Nyoyo Zangu, Haki ya Nani, Bandidu na Genge.

Filamu ambazo waigizaji wake wanawania tuzo ya waigizaji bora ni Bantu, Father Ezra, Safari ya Gwalu, Watatu, Bandidu, Heaven Sent, Genge, The Dream, Nyoyo Zangu, Mama wa Marehemu, Kivuli cha Ahadi na Malaika.
Tuzo zingine ni zile za mchekeshaji bora, Muziki bora na zingine.

Jaji Mkuu huyo alisema watazamaji wa Sinema Zetu wataendelea kupiga kura kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi na kutuma kwa namba 0757-339567.

No comments:

Post a Comment