Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 21 ya Jumuiya ya
Madola, ambayo ilitarajia kuagwa kesho Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa Jijini
Dar es Salaam, sasa itaagwa keshokutwa Jumatano, imeelezwa.
Habari za uhakika zilizopatikana leo zimesema kuwa timu hiyo
haitaagwa kesho kutokana na sababu zisizozuilika na badala yake itaagwa leo na
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Tayari Mkuu wa msafara wa timu hiyo, Dk Yussuf Singo, ambaye ni
Mkurugenzi wa Michezo nchini, aliondoka jana Jumapili kwenda Gold Coast kwa
ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuipokea timu ya Tanzania nchini
Australia.
Timu ya riadha itakuwa na Stephano Huche, Said Makula na Sarah
Ramadhani (marathon), Failuna Abdul (meta 10,000), Ali Hamisi Gulam (meta
100/200) na Anthony Mwanga (miruko na mitupo) wakati makocha ni Zacharie Barie
na Lwiza John.
Mabondia wa timu ya taifa wakianza na kumaliza mazoezi yao kwa sala kila siku. |
Ndondi ni Kassim Mbutike (kg 69), Ezra Paulo (kg 56), Haruna
Swanga (kg 91) na Seleman Kidunda (kg 75) na kocha wao ni Benjamin Moses.
Timu ya kuogelea inaundwa na Hilal Hilal na Sonia wakati kocha wao
ni Khalid Yahya Rushaka.
Timu ya mpira wa meza inaundwa na Amon Tumaini, Mtalaso, Neema
Mwaisyula na Fathiya Pazi wakati kocha wao ni Ramadhan Othman Suleiman.
No comments:
Post a Comment