Tuesday 20 March 2018

Brazil Kutumia Vifaa vya Spurs London

LONDON, England
TIMU ya taifa ya Brazil imesaini makubaliano na Tottenham Hotspur kutumia vifaa vya klabu hiyo ya Ligi Kuu kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia, limesema Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) juzi.

Mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia watakuwa wakifanya mazoezi mjini hapa kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Croatia Juni 3, kwenye uwanja wa klabu hiyo ya Uingereza,na Australia Juni 10 huko Vienna.

"Mbali na mechi hizo za kirafiki, tayari Brazil imeingia mkataba rasmi na Tottenham kwa ajili ya kushirikiana, ambapo watatoa vifaa vyao kuanzia Mei 28, ilisema taarifa ya CBF.

"Selecao (timu ya taifa ya Brazil) itatumia gym, bwawa la kuogelea na viwanja vizwili vya soka kwa ajili yao pamoja na jengo la hotel lililopo ndani ya eneo la mazoezi.

Brazil itaanza kampeni zake za kusaka taji la Kombe la Dunia kwa kucheza dhidi ya Uswisi Juni 17 kabla ya kukabiliana na Costa Rica na Serbia katika Kundi E.

Watacheza mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya wenyeji wa Kombela Dunia Urusi huko Moscow Ijumaa na mabingwa watetezi Ujerumani huko Berlin siku nne baadae.

No comments:

Post a Comment