Na
Mwandishi Wetu
KAIMU
Mkurugenzi wa Kiwanja CHA Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw.
Johannes Munanka amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na juhudi ili
kuongeza tija na kukuza uchumi wa nchi.
Bw.
Munanka alitoa kauli hiyo leo alipokutana na wafanyakazi wa JNIA, katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Transit uliopo Jengo la Kwanza la abiria (TBI), ambapo amesema
wafanyakazi wasipofanya kazi kwa bidii watashindwa kuzalisha kwa ziada. Huduma
kubwa inayotoa JNIA ni pamoja na kutua na kuruka kwa ndege za ndani na nje ya
nchi.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja
hicho, Bw. Johannes Munanka leo alipokuwa
akizungumza nao mambo mbalimbali ya kazi.
Amesema
wafanyakazi wasiofanyakazi kwa bidii watasababisha kuzorota kwa utoaji wa
huduma kwenye Kiwanja hiki, jambo ambalo litasababisha kukimbiza abiria na
wateja wengine wanaofanya shughuli zao mbalimbali kwenye kiwanja hiki, ambacho
ni miongoni mwa viwanja viwili vya Kimataifa vilivyopo nchini. Kiwanja kingine
cha Kimataifa ni cha Kilimanjaro (KIA).
“Ninawashukuru
sana wafanyakazi wanaochapa kazi kwa bidii bila kusukumwa ingawa wengine asili
ya kazi zao zinawasukuma kufanya hivyo, mfano mzuri ni waongoza ndege hawezi
kutegea, tofauti na wachache waliopo katika idara nyingine wamekuwa hawana
bidii ya kazi hadi wasukumwe,” amesema Bw. Munanka.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
Bw. Vedastus Fabian (mwenye miwani mbele) akiandika mambo mbalimbali
katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka leo.
Hata
hivyo, amesema wafanyakazi wote wanaosubiri kusukumwa waache mara moja na
wahakikishe wanajituma wenyewe, ili kuboresha huduma zinazopatikana JNIA,
ambazo zitakuwa sifa nzuri ya kuvuta wateja kutoka ndani na nje ya nchi.
“Ukiangalia
katika ngazi ya meneja au wanaoingia kwenye menejimenti nao wanatakiwa
kuwasimamia kwa umakini mkubwa na endapo watashindwa kufanya hivyo inanilazimu
nifanye kazi za kusimamia na umeneja, ambapo sio jambo zuri litasababisha
kushindwa kutekeleza majukumu mengine zaidi ya kiutendaji, hivyo ndugu zangu
tuchape kazi,” amesema Bw. Munanka.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka akijibu maswali ya
wafanyakazi wa kiwanja hicho, leo alipokutana nao katika mkutano uiliofanyika
katika ukumbi wa Transit ulipo Jengo la Kwanza la abiria (TBI).
Akizungumzia
vitendea kazi, Bw. Munanka ameahidi kushughulikia kwa ngazi ya JNIA ili
vipatikane haraka na pia kuwasilisha Makao Makuu (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania-TAA) vile vinavyohitaji idhini ya kuvinunua.
Ofisa Usalama, Bw. Musso John, akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoulizwa katika mkutano ulioitishwa na
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
Bw. Johannes Munanka uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Transit uliopo katika
Jengo la Kwanza la abiria (TBI).
No comments:
Post a Comment