Na Mwandishi Wetu
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa wa
Afrika Yanga wamejiweka katika nafasi ngumu ya kufuzu kucheza hatua ya makundi
baada ya kufungwa 2-1 na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa kwanza
uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo
hayo, mabingwa hao wa Tanzania Bara, sasa wanahitaji ushindi wa kuanzia angalau
mabao 2-0 na kuendelea.
Katika mchezo wa jana wageni waliandika bao la kwanza
katika dakika ya 11 kupitia kwa Lemponye Tshireletso aliifungia bao Township
bao la kuongoza baada ya kupiga shuti kali nje ya meta 18 lililokwenda moja kwa
moja wavuni.
Obrey Chirwa aliisawazishia Yanga katika dakika ya 30
baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Tshishimbi.
Yanga walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini
wachezaji wake hawakuwa makini na kukosa
mabao.
Katika dakika ya tatu, wapinzani wa Yanga nusura
wafunge baada ya Joel Morogorosi kutokuwa makini na mpira kuwahiwa na kipa wa
Yanga, Ramadhani Kabwili.
Ibrahim Ajib alikosa bao katika dakika ya 25 baada ya
kupiga mpira uliopaa juu ya lango la wapinzani wao hao kutoka Botswana.
Yanga ilianza kwa nguvu kipindi cha pili kwa kufanya
mashambulizi kadhaa, ambapo katika dakika ya 48 nusura wapate bao baada ya Gadiel Michael kushindwa
kufunga baada ya kupiga shuti kali lililopaa juu ya lango.
Timu hizo zitarudiana mjini Gaborone, Botswana Machi
17 katika mchezo wa utakaoamua timu ipi itinge hatua ya makundi huku Yanga
ikiwa na kibarua kigumu zaidi.
Nahodha wa Yanga, Pius Buswita akizungumza baada ya
mchezo huo jana alisema kuwa wapinzani wao walitumia vizuri nafasi walizopata, lakini
na wao wanaweza kushinda katika mchezo huo wa ugenini.
Kikosi cha Yanga: Ramadhani Kabwili,
Hassan Kessy, Gadiel Michael, Said Ali, Kelvin Yondan, Papy Tshishimbi, Pius
Buswita, Pato Ngonyani, Ibrahim Ajibu/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Emmanuel
Martine/Mwashiuya.
No comments:
Post a Comment