KAMPALA, Uganda
MUHUDUMU wa
katika ndege aliyeanguka kutoka katika mlango wa dharura wa ndege ya Emirates
iliyokuwa imeegeshwa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Entebbe, Uganda, amefariki
dunia, imeelezwa.
Mwanamke, ambaye
utaifa wake haujajulikana, alikimbizwa katika hospitali ya Kisubi kilometa 16 (sawa
na maili 10) kutoka eneo la tukio, alikufa mara baada ya kufikishwa hospitalini
hapo, ameeleza msemaji.
Ripoti hiyo
imesema kuwa mfanyakazi huyo wa ndege ya Emirates alikuwa akiiandaa ndege hiyo
kwa ajili ya kuchukua abiria wakati tukio hilo lilipotokea.
Mamlaka ya Anga
ya Uganda inasema kuwa imeanzisha uchunguzi.
Katika taarifa
yao imesema kuwa muhudumu huyo wa ndege “alikuwa akitaka kufungua mlango huo wa
dharura” na kwa bahati mbaya alianguka nje ya ndege, ambsyo ilitua na kupaki
salama”.
Msemaji wa
hospitali ya Kisubi Edward Zabonna alisema kuwa muhudu huyo wa ndege akiumia
katika “uso wake wote na magoti”.
Alisema kuwa
alikuwa “amepoteza fahamu lakini hai” wakati alipowasili hospitalini hapa juzi
jioni lakini alifariki muda mfupi baadae.
Taarifa kutoka
Shirika la Habari la AFP zilikariria taarifa kutoka katika ndege ya Emirates inayosema:
"Mfanyakazi wa ndege yetu bahati mbaya alianguka kutoka katika mlango wa
dharura uliokuwa wazi wakati akiandaa ndege kupandisha abiria”.
Ndege hiyo yenye
maskani yake Dubai ilimeahidi “kutoa ushirikiano mkubwa” kwa wachunguzi.
No comments:
Post a Comment