BARCELONA,
Hispania
KOCHA wa Chelsea,
Antonio Conte amesema kuwa timu yake inatakiwa “kuteseka” hapa kesho ikiwa inataka kufuzu kucheza hatua ya robo fainali ya
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Barcelona
inaikaribisha Chelsea leo katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 baada ya
kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Stamford Bridge mjini
London.
Chelsea ina
kibarua kigumu kwani inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao
2-2 ili kusonga mbele katika mashindano hayo makubwa ya klabu barani Ulaya.
Barcelona ilifunga
bao la kusawazisha katika dakika ya 75 kupitia kwa Lionel Messi kufuta bao la
kuongoza lililofungwa katika kipindi cha pili na kiungo Willian katika mchezo
wa kwanza mwezi uliopita.
Conte alisema
timu yake itakabiliana na kibarua kigumu dhidi ya mabingwa hao mara tano wa
Ulaya katika mchezo huo utakaofanyika Nou Camp.
"Tunatakiwa
kuwa vizuri sana lakini unapocheza dhidi ya timu kama hii, ambayo nafikiri ni
moja ya timu bora duniani, lazima ujiandae kutaabika, kama vile tulivyofanya
katika mchezo wa kwanza, ambako tulijiandfaa vizuri, “alise,a Conte katika mtandao wa klabu
hiyo.
"Hii sio ile
timu (Chelsea) yenye wachezaji wazoefu ambao wanacheza msimu wa kwanza au wa
pili katika Ligi ya Mabingwa.
"Lakini
tunatakiwa kucheza kama timu na na kujaribu kuwa tayari kutaabika, na katika
kila muda tunatakiwa kujua kuwa tunaweza kuwa na nafasi ya kufunga.”
Barcelona ilitawala
katika mchezo wa awali, lakini kikosi cha Conte kwa bahati mbaya hakikupata ushindi
baada ya Willian mara mbili kushindwa kufunga kabla ya mapumziko.
Barcelona imezidi
kuimarika kwa ajili ya mchezo huo baada ya nahodha wake, Andres Iniesta, ambaye
alikuwa nje ya uwanja kwa sababu ya maimivu, juzi alianza mazoezi kwa ajili ya
mchezo huo.
Iniesta alifanya
sehemu ya mazoezi pamoja na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Barca,
akiongeza matumaini ya kurejea katika mchezo huo wa marudiano wa hatu ya 16
bora.
Iniesta aliumia
Barcelona ilipocheza dhidi ya Atletico Madrid siku nane zilizopita na Jumamosi
alikosa mchezo walioshinda 2-0 dhidi ya Malaga.
Pia timu hiyo
Jumamosi ilimkosa nyota wake Lionel Messi, ambaye alikwenda kushuhudia kuzaliwa
kwa mtoto wake, Ciro, lakini mshambuliaji huyo atakuwemo katika mchzo huo.
No comments:
Post a Comment