LONDON, England
LIVERPOOL inapambana
ili kumbakisha mchezaji wake Mo Salah anayetakiwa na klabu kibao kwa ada ambayo
ni rekodi ya dunia ya pauni milioni 200.
Real Madrid,
Barcelona na Paris Saint-Germain (PSG) zote zinamtaka nyota huyo wa Misri kwa
fedha kibao.
Mchezaji huyo
amekuwa mpachikaji mzuri wa mabao msimu huu kwa Anfield, ambapo tayari
ameshafunga mabao 37 katika mechi 43 alizoichezea klabu hiyo.
Na hiyo ina maana
kuwa kocha Jurgen Klopp atakataa ada hiyo ya rekodi ili kuendelea kumbakisha
mchezaji huyo katika klabu hiyo.
Salah, ambaye
aliigharimu Liverpool kiasi cha pauni milioni 34.3 kutoka Roma katika kipindi
cha majira ya joto, akifananishwa na Lionel Messi na bao zake 28 katika
Ligi Kuu ikiwa na maana amefunga mabao matatu zaidi ya ligi zaidi ya
mchawi huyo wa Argentina.
Real itatupilia
mbali nia yake ya kumsajili Eden Hazard wa Chelsea endapo itamnasa Salah wakati
Barca tayari imeshapiga kelele kuhusu Mmisri huyo.
Swali ni je, Liverpool itaendelea kumbakisha Salah au itaweka mbele fedha kama ilivyofanya
kwa Coutinho.
No comments:
Post a Comment