Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amepongeza uwekezaji mkubwa
wa miuondo mbinu ya michezo uliofanywa na mwanariadha wazamani nchini Filbert
Bayi.
Dk Mwakyembe
aliyasema hayo jana alipotembelea maeneo mbalimbali ya Taasisi ya Fibert Bayi (FBF)
yaliyopo Mkuza, Kibaha, ambako kuna viwanja mbalimbali vya michezo vikiwemo
viwanja vya nje na ndani.
Mwakayembe baada
ya kufungua semina ya kuwawezesha wanawake kupitia michezo iliyofanyika Mkuza,
alitembelea maeneo hayo ya FBF na kushuhudia uwanja mkubwa wa ndani wenye viwango
vya kimataifa.
Sehemu ya uwanja
huo kwa sasa inatumiwa na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa meza ya
Tanzania itakayoshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Gold Coast,
Australia mwezi ujao.
Dk Mwakyembe
alisema kuwa hajawahi kufika Mkuza na wala hakujua kama kuna uwekezaji mkubwa kama
huo uliofanywa na Bayi, ambapo aliwataka akina Mbana Samatta kuiga uwekezaji wa
uliofanywa ma Bayi.
Alisema kuwa
wachezaji wengi wakipata fedha zaoe wamekuwa wakinunua magari ya kifahari
badala ya kuwekeza katika miundo mbinu mbalimbali kama alivyofanya Bayi na
kutengeneza ajira kwa watu kibao.
Mbali na uwanja
huo wa ndani ambao una viwanja vvya michezo yote ya ndani, pia kuna viwanja vya
nje vya soka, netiboli na mpira wa kikapu.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akiwa na mmoja wa wakufunzi wa semina ya kuwawezesha wanawake ndani na kupitia michezo aliyofungua jana Mkuza, Kibaha mkoani Pwani. |
Ukumbi mkubwa wa shughuli mbalimbali wa FBF Mkuza, Kibaha. |
No comments:
Post a Comment