Na Mwandishi Wetu, Karatu
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA) itadhamini Ngorongoro Marathon 2018 zitakazofanyika Aprili 21 kwa Sh
milioni 30.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka
Karatu, Arusha Mkurugenzi wa mbio hizo, Meta Petro alisema jana kuwa mamlaka
hiyo imekubali kudhamini mbio hizo zitakazofanyika Aprili 21 mwaka huu.
Petro alisema kuwa NCAA ndio mdhamini
mkuu wa mbio hizo, ambazo mwaka huu ni za 11 kufanyika tangu zilipoanzishwa na
zimekuwa zikikua mwaka hadi mwaka.
Alisema kuwa anatarajia mbio za mwaka
huu kushirikisha wanariadha wengi kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo
wakimbiaji mbalimbali nyota.
Mbali na NCAA, wadhamini wengine ni
Kampuni ya Vinywaji ya Bonite, ambao wamekubali kuendelea kudhamini mbio hizo
kwa kutoa bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni 15.
Petro alisema kuwa anawashukuru
wadhamini hao na bado milango iko wazi kwa wengine kujitokeza kusaidia
kudhamini ili kuzidi kufanikisha mbio hizo, ambazo zitaanzia katika lango kuu
la kuingilia na kutokea katika Hifadhi ya Ngorongoro na kumalizika katika
viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu.
No comments:
Post a Comment