Wanariadha wakichuana katika mbio za Tigo Kili Nusu Marathon leo mjini Moshi. |
Na Mwandishi Wetu, Moshi
WAKENYA wameendelea kutamba katika mbio za
Kilimanjaro Marathon kwa kilometa 21 na zile za kilometa 42 zilizofanyika leo mjini hapa na kushuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk
Harrison Mwakyembe.
Katika mbio za kilometa 42, Wakenya wameshikilia
nafasi 10 za kwanza kwa uoande wa wanaume na wanawake huku Failuna Abdil akiwa
Mtanzania pekee aliyekuwemo katika nafasi tatu bora kwa upande wa wanawake
katika mbio za kilometa 21 baada ya kushika nafasi ya pili kwa kutumia saa
01:13:52.
Waziri wa Habari,Utanaduni, Sanaa na Nichezo, Dk
Harrison Mwakyembe amesema kuwa amesononeshwa a matokeo ya mbio za Kilimanjaro
Marathon baada ya Tanzaniaa mmoja tu kuwemo katika tatu bora kati ya washindi
20.
Katika mbio za kilometa 21, Failuna Abdi alimaliza wa
pili nyuma ya Mkenya Flavious Kwamboka huku nafasi zingine zote katika 10 bora
zikichukuliwa na Wakenya ambao walitawala pia mbio za wanaume za kilometa 21
kuanzia nafasi ya kwanza hadi 10.
Mbali na mbio hizo za kilometa 21, Wakenya pia
walishika nafasi 10 za kwanza kwa upande wa wanajume na wanawake katika mbio za
kilometa 42 zilizoanzia na kumalizikia kwenye Uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Mwakyembe akizungumza baada ya kukabidhi zawadi kwa
washindi wa mbio hizo kwenye uwanja huo alisema kuwa lazima aseme ukweli na
hayuko tayari kuwapaka mafuta wakati matokeo hayajamfurahisha baada ya nafasi
zote za juu kuchukuliwa na Wakenya.
Aliwataja vijana wa Moshi kufanya mazoezi kwa bidii
ili mwakani waweze kulitoa taifa
kimasomaso kwa kufanya vizuri katika mbio hizo na kutwaa fedha zote zinatolewa
kwa washindi.
Mwakyembe alipongeza maandalizi mazuri ya mbio hizo
ambazo ni kubwa kabisa nchini kwa upoande wa marathon.
Grace Kimanzi wa Kenya alimaliza wa kwanza katika
mbio za kilometa 21 kwa kutumia saa 01:13:46 huku Failuna akitumia saa 01:13:52
huku mshindi wa pili tatu ni Mkenya Pauline Rkahenya aliyetumia saa 01:13:54
wakati kwa wanaume, Geofry Torotich wa Kenya alishinda mbio hizo kwa wanaume
kwa kutumia saa 01:03:26 na Simon Muthon alikuwa wa pili kwa saa 01:03:29.
Mshindi wa tatu katika mbio za kilometa 21 kwa
wanaume alikuwa Shadrack Korir aliyetumia saa 01:03:35, ambao walizawadia sh
mil 2, mil 1 na 650,000 kwa upande wa wanawake na wanaume.
Katika mbio za kilometa 42, Cosmas Muteti alimaliza
wa kwanza katika mbio hizo kwa kutumia saa 02:17:01, huku mshindi wa pili alikuwa
Eikana Yego aliyetumia saa 02:19:25 na George Onyancha aliyetumia saa 02:20:25.
Mwaka huu jumla ya washiriki wa mbio zote za kilometa
21, 42 na zile za kujifurahisha za kilometa tano,walikuwa zaidi 11,000.
No comments:
Post a Comment