Na
Mwandishi Wetu
TIMU ya
soka ya Taifa, Taifa Stars leo inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya DR Congo.
Stars
inacheza na Congo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-1 ilichopata toka
kwa Algeria wiki iliyopita katika mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Hemed
Morocco alisema wamejiandaa vema kwa mchezo huo baada ya kupoteza dhidi ya
Algeria pamoja na kwamba ana majeruhi wawili.
"Tumejiandaa
vizuri kwani ninajua Congo ni timu nzuri na sisi tunahitaji ushindi baada ya
kupoteza mchezo uliopita. Kikosi changu kina majeruhi Aishi Manula ambaye
anasumbuliwa na kifundo cha mguu na Abdulaziz Makame," alisema Morocco.
Naye
nahodha msaidizi wa Stars, Himid Mao alisema wao wamejiandaa kuhakikisha
wanawapa raha mashabiki kwani makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita
wameyafanyia kazi.
Kwa upande
wa Kocha wa DR Congo, Ibenge Florent alisema anaamini mchezo utakuwa mgumu
kwani Taifa Stars itakuwa inapambana kuhakikisha inashinda mbele ya mashabiki
wake huku akimtaja Simon Msuva na Mbwana Samatta kama wachezaji wanaowahofia.
"Tanzania
ni jirani zetu pia ni ndugu zetu ndiyo maana tumekubali kucheza nao. Mchezo
utakuwa mgumu kwani Taifa Stars haitakubali kufungwa kirahisi mbele ya
mashabiki wake na wachezaji Samatta na Msuva tunajua wakipata nafasi wanaweza
kufunga bao," alisema Ibenge.
Mchezo
huo unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni na viingilio ni Sh 5,000 VIP A na B, huku
maeneo mengine ikiwa ni Sh 1,000.
No comments:
Post a Comment