Mkurugenzi Mkuu wa MultiChoice, Maharage Chande. |
Na Mwandishi Wetu
WASANII wa
Tanzania wametakiwa kuwasilisha kazi zao kuanzia sasa hadi Aprili 30 kwa ajili
ya kushindania tuzo maarufu ya AMVCA 2018.
Mkurugenzi Mkuu
wa MultiChoice, Maharage Chande alisema jana, tuzo hizo za Africa Magic Viewers
(AMVCAs)wasanii wa filamu wanatakiwa kuwasilisha kazi zao kwa ajili ya
kushindanishwa.
Chande alisema
kuwa tuzo hizo, ambazo hufanyika kila mwaka zimekuwa zikihusisha maelfu ya
wasanii wa filamu kushindana.
Alisema kuwa tuzo
zilibuniwa ili kuthamini na kutambua mchango wa watengeneza filamu wa Afrika,
waigizaji, waigizaji na wataalam wa sekta ya filamu na telvisheni barani
Afrika.
Alisema kuwa tuzo
za mwaka huu zinatarajia kuwa kubwa zaidi na ushindani unatarajia kuwa wa aina
yake kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Alisema kuwa
baada ya kimya cha muda mrefu,
Africa Magic
ikishirikiana na MultiChoice, hatimaye wametangaza rasmi kuanza kwa kinyang’anyiro
cha moja ya tuzo maarufu duniani katika tasnia ya sanaa ya filamu.
Tuzo hizo ambazo
hufanyika kila mwaka zimekuwa zikihusisha mamia ya washiriki kutoka kila kona
ya bara la Afrika na zimekuwa moja ya tuzo zilizojizolea umaarufu mkubwa barani
Afrika na duniani kwa ujumla na limekuwa ni jukwaa muhimu la kutambua na kuenzi
vipaji vya tasnia ya filamu katika bara la Afrika.
“Baada ya mapumziko mafupi, tunayo furaha kutangaza kwamba mwaka 2018 utakuwa na toleo la mwaka wa sita
mfululizo wa MultiChoice na Africa Magic kuandaa AMVCAs kwa mafanikio na tunaendelea kujivunia
mabadiliko yanayoonekana kwenye nyanja ya filamu tangu Tuzo zilipoanzishwa.”
Katika msimu
uliopita, Filamu za Kitanzania ziliwika katika Kundi la Filamu Bora Afrika
Mashariki, ambapo “Aisha” ya Amil Shivji, “Naomba Niseme” ya
Staford Kihore, na “Homecoming” ya Seko
Shamte zilichaguliwa huku “Siri ya
Mtungi”
ikijitokeza kwenye Kundi la Filamu Bora za lugha ya Kiswahili.
Msimu uliopita,
filamu ya Kitendawili ya Richard Mtambalike ilinyakua tuzo ya filamu bora ya
lugha ya Kiswahili wakati Elizabeth Michael ‘Lulu’ alivuma
katika tuzo hizo katika filamu yake ya Mapenzi iliyoteuliwa kuwa filamu bora
kabisa Afrika Mashariki.
Kwa maelezo zaidi
juu ya mahitaji ya kujiunga na taratibu za uwasilishaji, tafadhali ingia www.dstv.com.
Kuingia AMVCAs ni
bure na tarehe ya kufungwa kwa maingizo ni 30 Aprili 2018. Filamu au sinema
zilizotayarishwa kwa ajili ya televisheni au tamthiliya za kwenye televisheni
ambazo ziliingizwa mwanzoni au kuteuliwa kwa ajili ya tuzo, au kutuzwa zawadi
katika shindano lingine la filamu na televisheni zinaruhusiwa kuingizwa kwenye
AMVCAs kama zinarushwa au kuoneshwa katika kipindi cha kuanzia Oktoba, 2016
hadi Machi, 2018.
Maelekezo ya
kushiriki:
HATUA YA 1
Prepare a 2 to 3
minute long showreel for your online submission. /Andaa ufupisho wa filamu yako
wenye muda wakati ya dakika 2 hadi 3 kwa ajili ya kuuwasilisha kwa njia ya
mtandao.
HATUA YA 2
Ingia
www.africamagic.tv na uende kwenye ukurasa wa kuwasilisha.
HATUA YA 3
Jaza fomu za uwasilishaji na upandishe video
yako. Namba ya kipekee ya utambulisho itatolewa kwa kila ingizo la mtandaoni
lililokamilika. Kisha kutegemea na eneo ulipo, tuma ingizo lake akionesha namba
zake za utambulisho.
No comments:
Post a Comment