ZURICH, Uswisi
Hatua hiyo ya kusogeza mbele mashindano hayo makubwa barani
Ulaya kwa timu za taifa, ilifikiwa jana Jumanne katika kikao cha dharura
kilichofanyika kwa njia ya video.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema jana na Chama cha Soka
cha Norway, mpango huo mpya umepanga mashindano hayo kufanyika kwa mwezi mmoja
kuanzia Juni 11 hadi Julai 11.
Uamuzi huo wa Uefa umetoa nafasi kwa ligi Ulaya kote kupata
nafasi ya kumaliza misimu yao pamoja na mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya
na Ligi ya Ulaya, baada ya kuodolewa kwa vikwazo ambavyo sasa wanaruhusiwa
kufanyika kwa mashindano hayo.
Hadi sasa hakuna utaratibu uliowekwa wa jinsi ya kufanyika kwa
mashindano hayo ambayo yamepangwa kufayika katika miji 12 ya Ulaya: Amsterdam,
Baku, Bilbao, Budapest, Bucharest, Copenhagen, Dublin, Glasgow, London, Munich,
Romena Saint Petersburg.
Nusu fainali za Ero zimepangwa kufanyika jijini London.
No comments:
Post a Comment