*Azama FC nao kibaruani Chamazi na Mbeya City
Na Mwandishi Wetu
YANGA mbayo imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, leo itaionesha Coastal Union makali yake wakati timu hizo zitakapokwaana kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, ndio viongozi wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 14 huku Azam FC ikishikilia nafasi ya pili katika msimamo.
Azam FC nao pia watashuka dimbani Chamazi Mbagala jijini Dar es Salaam abako watacheza na Mbeya City ya Mbeya katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wakusisimua.
Kwenye Uwanja wa Taifa Dar es
Salaam, Yanga itawakaribisha Coastal Union ya Tanga, huku Azam FC ikiwa mwenyeji
wa Mbeya City kwenye uwanja wao wa Chamazi, Mbagala.
Yanga wana
pointi 40 wakiwa tayari wameshacheza michezo 19 na kubakiza saba, wakati
Azam wana pointi 36 wakiwa wameshacheza michezo 18 na kubakiza minane,
wakitofautiana na vinara hao kwa tofauti ya pointi nne.
Kama Yanga ili waendelee kuwa
vinara wa ligi hiyo, wanahitaji kushinda mchezo wa leo. Halikadhalika, kwa
Coastal Union ambao wanazidi kushuka siku hadi siku wanahitaji kushinda ili
kujiepusha katika harakati za kushuka daraja.
Coastal Union ina pointi 24
ikiwa katika nafasi ya saba. Awali wakati wanaanza michuano ya ligi walikuwa
wakienda vizuri lakini walianza kupoteza mwelekeo baadaye na kujikuta wakishuka
kutoka nafasi ya tano hadi hiyo.
Timu hiyo ya Tanga imekuwa
haitishi kama zamani, kwani sasa hupoteza michezo yake ya nyumbani tofauti na
miaka iliyopita walikuwa wakiogopwa.
Katika mchezo wake wa hivi
karibuni, ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Aidha, katika mchezo wa
raundi ya kwanza dhidi ya Yanga, wagosi hao wa kaya walipokea kichapo cha bao
1-0, lakini huenda leo ikabadilika na kufanya vizuri ili kurejesha matumaini ya
kufanya vizuri katika mechi za mwisho za ligi hiyo.
Hata hivyo, Yanga leo
wanacheza na Coastal Union ikiwa chini ya kocha Jamhuri Kihwelo anayeinoa timu
hiyo kwa muda kumalizia mechi zilizobaki za Ligi Kuu.
Kwa upande wa Mbeya City
inayokutana na Azam FC, timu hiyo itakuwa na wakati mgumu kama itapoteza kwani
inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 24.
Pointi ilizonazo timu hii ya
Mbeya hazitoshi kuihakikishia kukwepa janga la kushuka daraja na hivyo
inahitaji pointi zote tatu ili angalau kujihakikishia usalama.
Na Azam pia wanahitaji
kushinda kwani nafasi yake itakuwa ngumu kama watapoteza kwa vile kuna
uwezekano wa kushuka kutokana na kutofautiana kwa pointi moja na Simba, ingawa
bado wana mechi nyingi kuliko Simba.
Katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Mbeya City ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya
Ndanda FC wakati Azam FC katika mchezo wake wa mwisho wa ligi walishinda 1-0
dhidi ya Coastal Union mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Timu zote zimekuwa zikitamba
kuondoka na ushindi katika mchezo wa leo, na kila moja ikionyesha shauku ya
kupambana ili kupata matokeo mazuri.
Msimamo:
P | W | D | L | GF | GA | +/- | Pts | |||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Young Africans | 19 | 12 | 4 | 3 | 28 | 11 | 17 | 40 | |||
2 | Azam | 18 | 10 | 6 | 2 | 25 | 12 | 13 | 36 | |||
3 | Simba SC | 21 | 9 | 8 | 4 | 27 | 15 | 12 | 35 | |||
4 | Kagera Sugar | 21 | 7 | 7 | 7 | 19 | 20 | -1 | 28 | |||
5 | Mgambo JKT | 20 | 8 | 3 | 9 | 17 | 19 | -2 | 27 | |||
6 | Ruvu Shooting | 21 | 6 | 8 | 7 | 14 | 18 | -4 | 26 | |||
7 | Coastal Union | 21 | 5 | 9 | 7 | 14 | 15 | -1 | 24 | |||
8 | Mbeya City | 20 | 5 | 9 | 6 | 15 | 17 | -2 | 24 | |||
9 | JKT Ruvu | 21 | 6 | 6 | 9 | 16 | 20 | -4 | 24 | |||
10 | Ndanda | 21 | 6 | 6 | 9 | 18 | 24 | -6 | 24 | |||
11 | Stand United | 20 | 6 | 6 | 8 | 17 | 23 | -6 | 24 | |||
12 | Mtibwa Sugar | 20 | 5 | 8 | 7 | 19 | 21 | -2 | 23 | |||
13 | Polisi Morogoro | 21 | 4 | 9 | 8 | 13 | 21 | -8 | 21 | |||
14 | Tanzania Prisons | 20 | 3 | 11 | 6 | 14 | 20 | -6 | 20 |
No comments:
Post a Comment