*Sumaye mgeni rasmi katika mbio za mwaka huu
Baadhi ya washiriki wa Ngorongoro Marathoni. |
Na Mwandishi Wetu
WANARIADHA kibao nyota wamethibitisha kushindana katika mbio za
Ngorongoro Marathoni, ambazo zitafanyika Jumamosi Aprili 18 zikishuhudiwa na
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Fredirick Sumaye.
Kwa mujibu wa mratibu wa wachezaji katika mbio hizo za kila mwaka,
Sumaye ndiye atakayekuwa mgeni rasmi ambapo ataanzisha mbio hizo katika lango
la kuingilia na kutokea katika mbuga na bonde la Ngorongoro.
Pia baada ya kuzianzisha mbio hizo ambazo mwaka huu zinatarajia
kushirikisha zaidi ya wanariadha 500 kutoka ndani na nje ya nchi, Waziri Mkuu
huyo wa awamu ya tatu ya uongozi nchini, atakabidhi zawadi kwa washindi kwenye
uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu.
Mary Naali atashiriki mbio za mwaka huu. |
Nyota Kibao
Kushiriki:
Petro alisema kuwa miongoni mwa wanariadha waliothibitisha
kushiriki mbio hizo ni pamoja na nyota waliounda timu ya taifa ya riadha
iliyomaliza ya sita katika mashindano ya dunia ya mbio za nyika huko, ambao ni
Bazil John, Ismail Juma, Joseph Panga, Alphonce Felix na Fabiano Sulle.
Mbali na hao pia bingwa wa mbio za Kilimanjaro Marathoni (kilometa
42) kwa upande wa wanawake mwaka huu Fabiola William, bingwa wa mbio za nyika
za taifa Catherine Lange, mkali wa mbio kibao nchini Failuna Abdi na Nathaeli
Elisante aliyeshika nafasi ya pili mwaka jana.
Kwa mujibu wa Petro wakali wengine watakaoshiriki mbio hizo ambazo
kila mwaka zimekuwa zikikuwa kwa kasi kubwa chini ya Zara Tanzania ni pamoja na
Fabian Joseph, Dickson Marwa, Pendo Japhet, Mary Naali na wengine wengi.
Dickson Marwa (kushoto) amethibitisha kushiriki mbio za mwaka huu. |
Zawadi kwa
Washindi:
Petro ambaye ni mwanariadha nyota wazamani wa Tanzania alisema
kuwa washindi wote mwaka huu watapata zawadi sawa bila kujali jinsi zao, tofuat
na mashindano mengi ambayo wanawake hupata zawadi kidogo ukulinganisha na
wanawaume
.
Mshindi wa kwanza kwa wanawake na wanaume, kila mmoja ataondoka na
kitita cha Sh. Milioni 1 wakati wa pili ataondoka na kiasi cha Sh. 500,000 na
watatu ni 250,000.
Alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yanafanyika chini ya udhamini
wa Zara Tanzania, Bonite, African Safari, Exim Bank, CRDB Bank, Marenga
Investment, Africa Safari, Hans Park,Red & White Wine.
Mtoto akivishwa medali baada ya kushinda mbio za kilometa 2.5. |
Lengo la Mbio
Hizo:
Awali, lengo kuu la kuendesha mbio hizo ambazo mwaka huu
zinakimbiwa kwa mara ya nane, lilikuwa ni kupiga vita ugonjwa wa malaria katika
jamii za wamasai.
Hatahivyo, baada ya lengo hilo kufanikiwa na ugonjwa huo kupungua,
mwaka huu lengo ni kuwaisaidia jamii hiyo katika tatizo la elimu na afya
ikiwemo ile ya uzazi.
Lazaro Nyarandu; Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na mmoja wa waratibu wa mbio hizo huku rais wa Riadha Tanzania (RT) (kushoto) Anthony Mtaka akishuhudia. |
No comments:
Post a Comment