MUNICH, Ujerumani
KIPA wa Bayern Munich Manuel Neuer anasema
mchezo wa Jumamosi dhidi ya Borussia Dortmund utakuwa kama fainali, licha ya
wapinzani wao kuchechemea katika ligi kwa sasa.
Bayern wanaongoza katika msimamo wa ligi
hiyo ya Ujerumani wakiwa pointi 10 dhidi ya Wolfsburg, wakati Dortmund wako
katika nafasi ya 10, Februari walikuwa wakishikilia mkia.
"Wakati wote timu hizi mbili zinapokutana
inakuwa kama fainali, ," alisema Neuer.
Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp alisema:
"amewekeza kila kitu kwa ajili ya mechi hii."
Kikosi hicho cha Klopp kimemaliza katika
nafasi mbili za juu katika misimu minne mfululizo, lakini sasa kinafukuzia
nafasi ya kucheza katika Ligi ya Ulaya kufuatia kutofungwa mechi saba baada ya
kuwa katika ukanda wa kushuka daraja.
Hatahivyo, Bayern itashuka uwanjani kucheza
na mpinzani wake huyo bila ya kuwa na wakali wake kama akina Franck Ribery, Arjen Robben na David
Alaba – lakini Klopp bado anahofia makali ya Bayern.
"Bayern watakuwa na Thomas Muller,
Mario Gotze na Robert Lewandowski katika safu ya ushambuliaji, " alisema kocha
huyo swa Dortmund.
"Hatufiki kuwa tuko katika kiwango
sawa kama Bayern. Lakini hatufikirii kama hatuna nafasi.
"Ingawa tuko katika nafasi ya 10,
tofauti ya pointi katika msimamo ni kubwa, hayo yamepita tugange yajayo, “alisema.
Nahodha wa Bayern Philipp Lahm anaweza
kuanza kwa mara ya kwanza tangu Novemba kutokana na maumivu.
"Hadi sasa nimekuwa nikifanya mazoei
kwa wiki nne mfululizo, na hiyo ikiwa na maana niko fiti, " alisema beki
huyo wa kutegemewa.
No comments:
Post a Comment