Thursday, 2 April 2015

Al-Shabab wavamia Chuo Kikuu na kuua 147 Kenya



NAIROBI, Kenya
WATU waliouawa katika shambulio la askari wa kiislamu wa al-Shabab katika Chuo Kikuu kaskazini ya Kenya imefikia 147, imesema serikali ya Kenya.

Zoezi la kuokoa eneo la chuo hicho kikuu cha Garissa sasa limemalizika, huku wavamizi wote wanne wakiuawa, kiliongeza chanzo hicho.

Taarifa hiyo ya serikali ilisema kuwa wanafunzi 587 wameokolewa, huku 79 wakijeruhiwa.

Majimbo manne karibu na mpaka wa Kenya na Somalia, Garissa, Wajir, Mandera na Tana River, yako katika uangalizi mkali kuwasaka magaidi wengine, ulisema uongozi kamati ya maafa.

Wanafunzi tisa walioumia vibaya wamekimbizwa kwa ndege kwenda katika hospitali ya mji mkuu wa Nairobi kwa ajili ya matibabu zaidi, waliongeza.

Uvamizi Ulivyotokea:
Watu wenye silaha waliovalia vinyago walivamia chuo kikuu mapema asubuhi Alhamisi.

1.  Askari waliingia katika eneo la chuo kikuu, na walinzi wawili walipigwa risasi na kuuawa.

2.  Mapigano yalianza ndani ya eneo la chuo
.
3.  Wanafunzi walivamiwa ndani ya madarasa yao wakati wakijiandaa kwa ajili ya mitihani.

4.  Watu wenye silaha walijitawanya katika mabweni ya wasichana.

5.  Baadhi ya wanafunzi walitoroka kupitia katika uzio wa chuo hicho.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki-moon alilaani uvamizi huo ambao aliuita "uvamizi wa kigaidi" na alisema UN iko tayari kuisaidia Kenya "kujilinda na ugaidi huo ".

Umoja huo wa Mataifa ulisema utatoa msaada kwa Nairobi ili kupambana na al-Shabab na kuendelea kufanya kazi kulishughulikia kundi hilo.

Serikali ya Kenya imemtangaza Mohamed Kuno, kiongozi wa ngazi za juu wa al-Shabab, kama mtu aliyepanga shambulio hilo la chuo kikuu.

Mtangazaji wa BBC wa Somalia alisema Bwana Kuno alikuwa mwalimu mkuu katika shule ya Kiislamu ya Garissa kabla hajajitoa mwaka 2007.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta a,itoa salamu zamaombolezi kwa familia ya watu walioathirika na ugaidi huo na kuagiza hatua kali za haraka kuchukuliwa mara moja na kuhakikisha mafunzo ya askari yanatolewa haraka.

'Milio ya Risasi'
Mapema, al-Shabab walisema wanachama wake walikuwa wakiwashikilia wakristo wakati waislamu waliwaachia huru.

Hatahivyo,haijulikana kama waliwaachia na kuwaruhusu kwenda wapi.
Iliripotiwa kuwa watu hao wenye silaha waliwaamrisha wanafunzi kujilaza sakafuni lakini badhi yao walipata mwanya wa kutoroka.

Mwanafunzi Augustine Alanga alisema: "Hali ilikuwa mbaya, kwani milio ya risasi ilikuwa kila mahali."

Alisema ilikuwa jambo la kushangaza kwa chuo kikuu kulindwa na polisi wawili tu.

Mwanafunzi Collins Wetangula alisema wakati watu wenye silaha wakiingia hosteli aliweza kuwasikia wakifungua milango na kuuliza watu waliondani kama Waislamu au Wakristo.

"Ikiwa weweni Mkristo walikupiga risasi hadharani…”alisema.

Al-Shabab katika taarifa yao walisema kuwa walikivamia chuo kikuu hicho kwa sababu wana ugomvi na Kenya
.
Oktoba mwaka 2011 Askari wa Kenya waliingia Somalia kwa ajili ya ujaribu kuwapiga askati wa Boko Haramu.

No comments:

Post a Comment