Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ndondi Tanzania (BFT) limeteua mabondia 17
watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya Michezo ya Afrika na mingine ya
kimataifa, imeelezwa.
Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema kuwa, mabondia hao
waliteuliwa katika mashindano ya kimataifa yaliyomazika hivi karibuni kwenye
Uwanja wa Ndani wa Taifa na kushirikisha na mabondia wa Kenya na Uganda.
Alisema kuwa mashindano hayo yaliyofanyika Uwanja wa Ndani,
yalikuwa na mafanikio makubwa na yalimaliziaka Jumamosi.
Mabondia waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa
katika timu zao zinafanyika na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa
kuanza mazoezi kabla ya tarehe 15.04.2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano
mbalimbali ya kitaifa.
Michezo ya Afrika itafanyika Brazzavile, Kongo kuanzia Septemba 4-19,
mashindano ya ubingwa wa dunia ya Aiba Oktoba 5-18 Doha Qatar.
Mabondia
waliochaguliwa kwa uzito wao ni kama ifuatavyo:-
49 kgs L/FLY
• Mohamed Mzeru –JKT
• Maulid Athumani-
• Ibrahim Abdalah –
Magereza.
52 Kgs Fly
Weight.
• Juma Ramadhani- Temeke
• Said Hofu- JKT
56 Kgs Bantam
Weight
• Ahamad Furahisha- JKT
• Bon Mlingwa- JKT
60 Kgs Light
weight.
• Elias Mkomwa- JKT
• Bosco Bakari-
JKT
• Fabian Gaudence- NGOME
64 Kgs Light
Weight
• Kassim Mbwitike- JKT
69 Kgs.
Welter Weight.
• Said Gulushad – JKT
• Seleman Bamtulah- JKT
75 Kgs Middle
Weight.
• Ivan Mussa –
Kagera
81 Kgs light
Heavy
• Hamidu Halfan-JKT
91 Kgs Heavy
weight
• Alex Sitta- JKT
• Nuru Ibrahim- Magereza
Aidha, BFT inawapongeza mabondia
wote kwa jitihada kubwa walizofanya na hatimae kuchaguliwa kuwa mabondia wa
timu ya taifa ya ngumi 2015.
No comments:
Post a Comment