Mwanamke wa Misri Sisa Abu Daooh (kushoto), akipokea tuzo kutoka kwa rais wa nchi hiyo, Abdel-Fattah El-Sissi. |
CAIRO, Misri
KWA zaidi ya
miongo minne (miaka 40), mama wa Misri Sisa Abu Daooh amekuwa akivaa kama
mwanaume ili kumuwezesha kupata ajira kwa ajili ya kupata fedha za kuendeshea familia yake.
Mama huyo
wiki iliyopita alizawadiwa tuzo ya "woman breadwinner" na serikali
huko kwao Luxor na kupongezwa na rais wa Misri.
Abu Daooh,
65, wiki iliyopita alikuwa katika sherehe iliyofanyika katika makazi ya rais, ambako
alikutana na Rais Abdel-Fattah El-Sissi na kupokea zawadi ya fedha ya kiasi cha
dola za Marekani 6,500.
Akiwa
amevalia joho la kiasili la kiume na kilemba wakati akipokea tuzo hiyo, ambapo
alipongezwa na rais kama "mwanamke mfanyakazi asiyewakawaida."
Abu Daooh alikuwa
na ujazito na mtoto wakike Houda wakati mume wake alipofariki dunia katika
miaka ya 1970, akimuacha ndiye mtunzaji wa familia.
Abu Daooh alibaini
haraka kuwa katika tamaduni za jamii ya Kimisri wakati huo, kulikuwa na nafasi
chache sana za kufanya kazi kwa wanawake wasio na elimu kama yeye, na alikuwa
rahisi kupata kazi ukiwa umevaa kama mwanaume.
Mama huyo
baada ya kuvaa kama mwanaume alipata kazi katika sehemu ya kutengenezea
matofali na kung’arisha viatu, na aliamua kuvaa
hivyo ili kukwepa kunyanyapaliwa.
"Ili
kujilinda mwenyewe nisinyanyaswe na wanaume na kusakamwa kutokana na tamaduni
zetu…niliamua kuvaa kama mwanaume na
kufanya kazi pamoja nao katika kijiji kingine ambako hakuna aliyekuwa akinijua,
” aliuambia mtandao huo.
Hadi sasa, Abu
Daooh bado anfanyakazi mbali na nyumbani kwao. Mume wa mtoto wakike wa Abu
Daooh hawei kufanyakazi, hivyo mama huyo anaendelea kutafuta kipato kwa ajili
ya familia yake.
“Mama yangu ni
mmoja ambaye anaihudumia familia, " alisema mtoto wakike wa Abu Dooah.
"Kila
siku anaamka saa 12 asubuhi na kuanza kung’arisha viatu huko Luxor. Nambebea vitu vya kufanyia kazi kwa sababu sasa
ni mtu mzima.”
Abu Dooah alisema
mama amekuwa akivaa nguo za kiume, na amesisitiza katika kipindi kilichobaki
cha maisha yake ataendelea kuvaa nguo hizo. “Nimeamua kufaa katika nguo hizi.
Katika maisha yangu yaliyobaki nitavaa nguo hizi, ” aliliambia gazeti moja.
No comments:
Post a Comment