ABUJA, Nigeria
MSHINDI wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu nchini Nigeria, Muhammadu Buhari, amepongeza ushidi wake kama ni kura ya mabadiliko na kudhihirisha ameleta demokrasia.
Bw. Buhari pia amempongeza rais anayemaliza muda wake Goodluck Jonathan kama "mpinzani wa thamani " ambaye amekubali kushindwa katika uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi.
Jenerali Buhari alimbwaga Bw. Jonathan kwa kupata kura za ndio milioni 15 huku mpinzani wake ambaye ni rais wa sasa alipata kura milioni 12.9.
Waanfgalizi wa kimataifa kwa ujumla wamepongeza uchaguzi huo, ingawa kulikuwa na tetesi za kutokea kwa vurugu.
Bw. Buhari, wa chama cha All Progressives Congress (APC), amekuwa mgombea wa kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi nchini Nigeria.
Kiongozi huyo wazamani wa kijeshi katika hotuba yake leo Jumatano baada ya ushindi alielezea ushindi wake kuwa ni wa kihistoria.
No comments:
Post a Comment