Na Mwandishi Wetu
PAMOJA na kupokea kichapo cha bao 1-0
kutoka kwa wenyeji wao wa Zimbabwe FC Platinum, Yanga ya Tanzania imefanikiwa
kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la
Afrika.
Kikosi hicho cha Yanga kinachonolewa na
kocha Mholanzi Hans van der Pluijm kimefanikiwa kutinga raundi ya pili ya
michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika(CAF),kwa
ushindi wa jumla ya mabao 5-2.
Bao pekee la FC Platinum hilo lilifungwa katika
dakika ya 29 na kiungo Walter Musona, aliyeunganisha krosi ya Brian Muzondiwa
akiwa ndani ya eneo la hatari la Yanga na kufanya uwanja wa Mandava uliopo
Bulawayo kulipuka kwa shangwe za wachimba Almasi wa Zimbabwe.
Pamoja na Platinum kuanza mchezo huo kwa
kasi lakini wachezaji wa Yanga walionekana kucheza kwa kujitolea na umakini
mkubwa huku wakifanya mashambulizi ya kustukiza.
Mrisho Ngassa alipoteza nafasi ya wazi
dakika ya 22 baada ya shuti alilopiga kupanguliwa na kipa wa Platinum Petros
Mhari, hiyo ikiwa baada ya kupokea mpira wa kichwa wa Amissi Tambwe aliyekua
ameunganisha kona iliyochongwa na Simoni Msuva.
Vijana wakocha Norman Mapeza walikwenda
mapumziko wakiwa hawana furaha baada ya lengo lao la kupata mabao angalau
matatu kushindikana na kuendelea kubaki katika wakati mgumu kutafuta mabao
manne kipindi cha pili.
Kipindi cha Pili Platinm waliendelea
kupambana wakijaribu kutengeneza mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga,lakini
ngome ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na nahodha wake Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na
Mbuyu Twite ilikuwa imara kuondoa hatari zote langoni mwao.
Yanga ilionekana kuzinduka mwishoni mwa
mchezo huo na kupoteza nafasi mbili za wazi ambazo washambuliaji wake Amissi
Tambwe na Msuva walizipata katika dakika za 77 na 84.
Hiyo inakuwa ni mara ya pili kwa kocha wa
Yanga kushindwa kupata ushindi inapocheza ugenini kwenye michuano ya Kombe la
Shirikisho mwaka huu mara ya kwanza licha ya kuitoa BDF XI ya Botswana, lakini
mechi ya marudiano iliyochezwa Lobatse Botswana ilifungwa mabao 2-1 na kufuzu
raundi ya kwanza kwa matokeo ya jumla ya 3-2 na sasa imefungwa 1-0 Ugenini
kwenye uwanja wa Mavanda Zimbabwe.
Kwa matokeo hayo, Yanga itacheza na mshindi
kati ya Benfica de Luanda ya Angala au Etoile du Sahel ya Tunisia.
Yanga:Ally
Mustaph,Juma Abduli, Oscar Joshua,Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Said Juma/Kelvin
Yondan, Salum Telela,Simon Msuva/Danny Mrwanda, Haruna Niyonzima,Amissi
Tambwe,Mrisho Ngassa.
No comments:
Post a Comment