JARKATA, Indonesia
SERIKALI ya Indonesia usiku wa kuamkia leo
imewaua kwa kuwapiga risasi wauzaji nane wa madawa ya kulevya baada ya watu hao
kuhukumiwa kifo.
Hukumu hiyo imetekelezwa na kikosi maalum cha
kuwapiga wafungwa risasi, licha ya wito kutoka kwa mataifa mbalimbali duniani
kutaka watu hao wasinyingwe.
Wafungwa hao walikuwa tisa, lakini kuuawa kwa
raia mmoja wa Ufilipino, Mary Jane Veloso, kumecheleweshwa baada ya mwanamke
mmoja kujiwasilisha kwa polisi Nchini Ufilipino, akisema kuwa ndiye aliyemhadaa
mfungwa huyo mwanamke mwenzake, kupeleka dawa za kulevya Indonesia.
Andrew Chan (kulia), na Myuran Sukumaran (kushoto) ambao waliuawa usiku wa kuamkia leo. |
Aidha, raia wawili wa Australia Andrew Chan,
31, na Myuran Sukumaran, 33, walinyongwa pamoja na wafungwa wengine sita na
kikosi hicho maalum cha kuwaua wafungwa.
Raia hao wa Australia ndio walikuwa wa kwanza
kuuawa baada yam lo wa usiku.
Inaelezwa kuwa Chan – ambaye aliukumiwa kifo
mwaka 2005 kwa kupanga mpango huo unaoitwa `Bali Nine heroin smuggling plot’ –aliukumiwa kifo miaka miwili
iliyopita.
Waaustralia wawili waliouawa na kikosi maalum cha kuua wafungwa usiku wa kuamkia leo. |
Chan,ambaye mapema mwaka huu gerezani, alibatizwa
na kuwa Mkristo alisema kuwa, Sandiford muda mfupi kabla hajahamishiwa katika
kisiwa hicho cha mauaji, alitubu dhambi zake.
Alisema kuwa: 'Siogopi kufa lakini anahofia
kufa taratibu. Naogopa risasi na naogopa kwa kuwa hakitakuwa kifo cha haraka. '
Sandiford alihukumiwa kifo huko Bali tagu
alipopatikana na hatia ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya
pauni Milioni 1.6 za cocaine kupitia uwanja wa ndege wa kisiwani mwaka 2012.
Mwanamke Muindonesia ambaye kifo chake
kimeahirishwa alisema kuwa alisafirisha dawa hizo ili kuwalinda watoto zake,
ambao usalama wao uliuwa hatarini.
Serikali ya Uingereza ilikataa ombo la
kumlipia Sandiford ada ya kisheria kwa ajili ya rufaa yake.
Usiku, yalionekana magari ya wagonjwa yakiwa
yamebeba majeneza ya Chan na Sukumaran yakiwasili katika 'kisiwa cha kifo' ambako
walipigwa risasi na kuuawa.
Picha tofauti zinaonesha jinsi watu waliokumiwa kifo wanavyoandaliwa hadi kuuawa. Picha namba sita inaeleza kuwa, daktari endapo atathibitisha kuwa mfungwa baada ya kupigwa risasi lakini bado ana dalili ya uhai, basi kamanda wa maaskari hao wauaji anammalizia mfungwa huyo kwa kumpiga risasi kichwani kwa kutumia bastola yake. |
Familia ya Chan na Sukumaran ilitoa taarifa
kufuatia kuuawa kwa ndugu zao hao.
'Leo tumewapoteza Myuran na Andrew. Watoto
wetu, kaka zetu, ' walisema katika taarifa hiyo.
'Miaka kumi tangu walipokamatwa, walifanya
kila lililowezekana ili waachiwe, na kuwasaidia wengine, lakini
hawakusikilizwa.’
Mary Jane Fiesta Veloso (katikati), ambaye kifo chake kiliahirishwa baada ya mwanamke mmoja kujisalimisha nchini Ufilipino, akisema kuwa yeye ndiye aliyemdanganya dada huyo kubeba dawa hizo za kulevya. |
No comments:
Post a Comment