Dereva taxi India ahukumiwa kwa kumbaka abiria wake
DELHI, India
MAHAKAMA ya nchini India leo muda mfupi uliopita imemkuta
na hatia dereva taxi wa `mtandaoni’
kwa kosa la kumbaka abiria wake mwanamke mwaka jana, imeelezwa.
Shiv Kumar Yadav pia alikutwa na kosa na jinai la
kutishia na kuteka, alisema mwendesha mashtaka wa Serikali. Alikana mashataka
hayo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26 alichukuliwa
na kupelekwa mahali pasipo julikana ambako alibakwa baada ya kuboku safari yake kwa
kutumia mtandao akiwa nyumbani Desemba mwaka jana.
Delhi baadae ilipiga marufuku utaratibu wa kukodi
taxi kwa kutumia simu au mitandao mingine ya mawasiliano kutokana na
matukio ya kialifu.
Hatahivyo, kampuni hiyo iliomba radhi kwa tukio
hilo na kubainisha kuwa iko tayari kuweka utaratibu mpya na bora zaidi.
Mwanamke huyo pia alifungua kesi katika mahakama ya
Marekani dhidi ya huduma hiyo, ambayo baadae ilimalizwa nje ya mahakama.
Vitendo vya ubakaji vimekuwa vikifuatiliwa kwa
karibu nchini India tangu mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 kubaka na
kunyongwa katika basi jijini Delhi Desemba mwaka 2012, ambapo jumuiya ya
kimataifa kutaka sheria kali kuhusu vitendo vya ngono na vurugu.
No comments:
Post a Comment