Kundi la wasichana wa Nigeria waliotekwa na Boko Haram kutoka kijiji cha Chobok mwaka 2014. Bado haijathibitishwa kama wasichana hao waliookolewa ni wale kutoka Chibok. |
LAGOS, Nigeria
JESHI la Nigeria
limewakomboa wasichana 200 na akina mama 93 ambao walitekwa na kundi la kigaidi
la Boko Haram.
Hilo lilitokea wakati wa
zoezi la kijeshi kuurejesha msitu wa Sambisa uliopo kaskazini ya Nigeria kutoka
kwa kundi la kijeshi la Kiislamu.
Hatahivyo, ilithibitishwa
kuwa watu hao waliookolewa sio wale wasichana wakiwemo wanafunzi 300 Wakristo
waliotekwa mwaka jana huko hibok na kundi hilo.
Jeshi liliweka katika ukurasa wao wa Twitter
taarifa ikisema: 'Jeshi mchana huu iliwaokoa wasichana 200 na akina mama 93
kutoka msitu wa Sambisa.
'Hatuwezi kuthibitisha kama wasichana wa Chibok
wamo katika kundi hili la watu walookolewa,' ilisema taarifa hiyo, ikiongeza
kuwa jeshi la Nigeria pia limeharibu kambi tatu zinazoendeshwa na askari hao wa
Boko Haram.
Baada ya kutekwa na Boko Haram, baadhi ya wasichana walionekana katika picha wakiwa wamevalishwa mavazi marefu ya hijab. |
Wanadiplomasia na wapigania haki za binadamu
wamesema kuwa wanaamini kuwa wasichana hao walikuwa wakishikiliwa msituni
umbali wa karibu maili 60 kutoka Chibok.
Jeshi la Nigeria likisaidiwa na ndege za
kivita lilivamia msimu huo ambao ni eneo la zamani la msimu wa hifadhi la
kikoloni mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni sehemu ya zoezi la kutaka
kulipokonya jimbo hilo kutoka kwa Boko Haram.
Kanali Sani Usman alisema: 'Jeshi liliokoa
wasichana 200 na wanawake 93.
'Hatahivyo, sio wale kutoka Chibok, kijiji
ambacho zaidi ya wasichana 200 walitekwa Aprili mwaka 2014.
'Hadi sasa, (jeshi) limeharibu na kufagia
kabisa Sassa, Tokumbere na kambi zingine mbili katika eneo la Alafa, zote
zikiwa katika msitu wa Sambisa.
Taarifa hiyo ilisema kuwa wasichana na akina
mama hao watafanyiwa vipimo vya afya ili kujua kama walitekwa nyara au kuolewa
na askari hao wa Boko Haramu.
'Kesho pia watahojiwa kujua kama walikuwa ni
wake wa askari wa Boko Haram, kama wanatoka Chibok, au wako kwa muda gani
katika kambi, na kama wana watoto.
Boko Haram waliteka wanafunzi wakike 200 karibu
na kijiji cha Chibok Aprili mwaka jana, ambapo jumuiya ya kimataifa imelaani
kitendo hicho.
Wanafunzi hao walichukuliwa katika malori
usiku wa Aprili ya tarehe 14 na 15, abaada ya magaidi kutoka Boko Haram-wakidai
kuwa elimu ya Magharibu ni dhambi’-na walivunja shule kwa kujidai kuwa wao ni walinzi.
Wanafunzi hao walilazimishwa kubadili dini na
kuwa Waislamu na kuolewa na wanajeshi wa kundi hilo.
Dunia nzima ililaani uvamizi huo na kufanya
kampeni kubwa inayojulikana kama '#bringbackourgirls' – lakini zaidi ya 200 bado
hawajapatikana huku wengine wakidhaniwa kuwa waliachiwa au kuuawa.
Wiki iliyopi Nigeria niliadhimisha mwaka
mmoja tangu kupotea kwa wasichana hao huku rais mpya wan chi hiyo Muhammadu
Buhari, aliyeshinda uchaguzi wa urais wiki mbili zilizopita, alisema kuwa
watafanya kila njia kuhakikisha wasichana hao wanarejeshwa nyumbani.
'Serikali yangu itafanya kila iwezalo
kuwarejesha nyumbani wasichana hao, ‘ aliongeza rais huyo.
No comments:
Post a Comment