CANBERRA,
Australia
MAMA mmoja
nchini Australia amekuwa akipambana ili kupona maambukizo ya ngozi, ambayo
yanatishia maisha yake na kumuacha akiwa nusu amepooza.
Tatizo hilo
alilipata baada ya kuazima brashi ya `makeup’.
Gazeti la
The Daily Mail la Australia liliripoti kuwa Jo Gilchrist Siku ya Wapendao ndio alianza
kujisikia maumivu katika mgongo wake na baadae maumivu hayo yaliongezeka na
kujisikia vibaya zaidi ya maumivu anayopata mama wakati wa kujifungua.
Baadae mdada
huyo alianza kupoteza hisia katika miguu yake na sehemu ya chini ya mwishi na
kukimbizwa hospitali kwa kutumia ndege hadi Brisbane kwa ajili ya kufanyiwa
upasuaji wa dharura.
Inaelezwa
kuwa maambukizi hayo yalipatikana baada ya kutumia brashi ya kujipambia ya
rafiki yake kwa ajili ya kuziba chunisi usoni.
Jo
Gilchrist, 27, aliachwa amepooza kutokana na maambukizo hayo ya ngozi
aliyoyapata kutoka katika brashi ya rafiki yake ya kujipambia.
“Rafiki yangu
alikuwa na maambukizo usoni mwake na mimi nilitumia brashi yake” alisema dada
huyo. Sikujua kama hilo litatokea. Nilikuwa naazima brashi za wenzangu mara kwa mara."
Maambukizo
hayo yameharibu kabisa uti wa mgongo, na madaktari walisema kuwa dada huyo hatatembea
tena. Lakini Gilchrist, 27, amekuwa akifanya kazi kuthibitisha kuwa madaktari
hawakuwa sahihi, na ameenda kufanya mazoezi ili kujaribu kuponya miguu yake.
"Ni
hali ngumu ambayo sijawahi kukutana nayo," aliandika katika ukurasa wake
wa Facebook. "Nimekuwa nikilala sana usiku na mchana na kupata maumivu
kibao.”
Matibabu ya
nguvu kupitia mazoezi yamemsaidia kuanza kusogeza miguu yake taratibu, kusimama
na kupiga hatua chache wakati wa mazoezi hayo.
No comments:
Post a Comment