Na Mwandishi Wetu
TUME ya Uchaguzi (NEC) imesema haitoweza kuendelea na zoezi la
kura ya maoni kama ilivyopangwa kufanyika Aprili 30, kutokana na kutokamilika
kwa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji
Mstaafu Damian Lubuva (pichani) amesema kuwa zoezi lolote la kupiga kura likiwepo la kura
ya maoni ya Katiba inayopendekezwa linategemea kuwepo kwanza kwa daftari la
kudumu la wapigakura.
Licha ya kutangaza kuhairishwa zoezi la upigaji kura ya maoni hadi
baadae, Jaji Lubuva amesema zoezi la uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga
kura litaendelea katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Iringa na Mtwara.
No comments:
Post a Comment