KATHMANDU, Nepal
ANGALAU watu 3,218 sasa wanafahamika kuwa
wamekufa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchi Nepal Jumamosi,
imeelezwa.
Kiongozi wa wakala wa majanga na maafa wa
Nepal, Rameshwor Dangal alisema kuwa watu wengine 6,500 wamejeruhiwa kutokana
na madhara yaliyotokana na tetemeko hilo la ardhi.
Pia watu kibao wameripotiwa kuuawa katika
nchi za jirani za China na India.
Maelfu ya watu walitumia usiku wa pili nje
baada ya tetemeko lenye ukumbwa na magnitude 7.8, ambalo pia liliua katika
mlima wa Everest lilitokea.
Taarifa zinasema kuwa vikosi vya uokoaji nchini
humo vimezidi kuimarishwa baada ya kutokea kwa tetemeko hilo.
Kwa mujibu wa maofisa nchini humo, tetemeko
hilo ni kubwa na limesababisha madhara makubwa, ambayo hayajawahi kutokea kwa
muda wa miaka 80 sasa.
Tayari nchi nyingi na mashirika ya misaada
yamejitokeza kusaidia wale wote walioathirika na tukio hilo lililochukua uhai
watu na kuharibu majengo na mali zingine.
Zaidi ya watu 17 walipoteza maisha katika
Mlima Everest baada ya kuanguka kwa theluji.
Theluji hiyo pia ilisababisha maafa katika
maeneo mengine jirani na Nepal kama India na Bangladesh.
Tetemeko lenye ukubwa wa magnitude 6.7
lilisikika Mashariki mwa Nepal katika Jiji la Kathmandu na kusababisha taharuki
baada ya watu kuanza kukimbia bila mpangilio.
Kutokana na tetemeko hilo,theluji katika mlima
huo wa Everest lilianza kuanguka na kusababisha madhara hayo katika maeneo tofauti
tofauti yanayouzunguka mlima huo.
Baada ya tetemeko hilo kubwa muda mfu;I baadae
lilifuatia tetemeko lingine lenye ukubwa wa magnitude 6.6. Jumapili asubuhi
lilitokea jingine Nepal lenye ukumbwa na magnitude 6.7.
Taarifa zaidi kutoka nchini humo ziliongeza
kuwa, idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo, imeongezeka baada ya maeneo
mengi ya vijijini kushindikana kupatikana kwa taarifa kamili za vifo na
majeruhi.
Pamoja na vifo na uharibifu huo mkubwa wa
vitu na mali, matetemeko hayo yamesababisha kukatika kwa mawasiliano nchini humo,
zikiwemo barabara kukatika na milima kuporomoka.
Zaidi ya watu 700 wamepoteza maisha jijini
Kathmandu pekee, huku miili mingi ikisafirishwa kwa boti na kuhifadhiwa katika
hospitali mbalimbali jijini humo.
No comments:
Post a Comment