*Yaiombea Azam ifungwe na Stand United na wao waichape Ndanda
Kikosi cha Simba. |
Na Mwandishi Wetu
LIGI Kuu Tanzania Bara imefikia patamu wakati
Yanga ikibakisha pointi tatu tu kutangaza ubingwa, vita kali inayoendelea ni ile ya kuwania kuwania nafasi ya pili kati ya mabingwa watetezi Azam FC pamoja na Simba.
Azam FC leo wanacheza na Stand United ya Shinyanga
kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Mbagala wakati Simba leo watakuwa wenyeji
wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba inayoshuka dimbani leo, endapo itafungwa na Ndanda FC ya Mtwara na
Azam FC ikiifunga Stand United, basi wekundu hao wa Msimbazi watakuwa wameondolewa
katika mbio hizo za kusaka nafasi ya pili.
Simba ikifungwa leo itakuwa na uwezo wa
kufikisha pointi 44 huku Azam FC endapo itashinda leo itakuwa imefikisha pointi
45, ambazo hata kwa dawa haziwezi kufikiwa na wekundu hao wa Msimbazi.
Simba wenyewe kwa sasa wanasaka nafasi ya
pili ili kupata kuliwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la
Afrika.
Kimsimamo kabla ya mchezo wa leo, Azam
imecheza mechi 22 na hivyo kubakisha nne na ikishinda zote itaweza kufikisha
pointi 54, ambazo Yanga itazipita endapo itashinda mchezo wake wa Jumatatu
dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Azam leo ikishinda itafikisha pointi 45 na
itabakisha pointi tatu ili kufikisha 48 na kuiweka kando kabisa Simba katika
mbio hizo za kusaka nafasi ya pili, kwani uwezo wa Simba ikishinda mechi zote, itafikisha
jumla ya pointi 47 tu.
Aidha, Mbeya City itawakaribisha Kagera Sugar katika mchezo utakaochezwa
kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Simba inahitaji kushinda mchezo huo kama
kweli inahitaji kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, lakini bado ina
changamoto kama Azam watashinda kwani nao pia wanatafuta ushindi ili kugombania
taji au kuendelea kubaki katika nafasi hiyo.
Simba na Azam Fc zinatofautiana kwa pointi
nne, mmoja akishinda na mwingine akashindwa kuna atakayeshuka na mwingine
kupanda kwa vile tofauti ya pointi itakuwa ndogo hivyo, kila timu inahitaji
ushindi kuhakikisha inaendelea kutetea nafasi ilizonazo.
Timu ya Ndanda FC ambao katika mchezo wa
raundi ya kwanza walifungwa na Simba mabao 2-0 uliochezwa Nangwanda Sijaona,
wako katika hali mbaya, kwani wanashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi
wakiwa na pointi 25.
Iwapo watashindwa kuonyesha juhudi katika
mchezo huo watazidi kuwa hatarini kwasababu tayari wameshacheza michezo 23 na
wamebakiza mitatu kuanzia wa leo hivyo ushindi ni muhimu kwao.
Mabingwa watetezi Azam FC licha ya kujifariji
kuwa wana nafasi ya kutetea ubingwa wao, pia wanahitaji kuonyesha juhudi kwa
vitendo ili kufanya vizuri.
Kikosi cha Azam FC. |
Azam FC wamekuwa wakisuasua katika baadhi ya
mechi zao zilizopita na hivyo kuachwa kwa pointi na vinara wa ligi Yanga.
Timu wanayokutana nayo Stand United licha ya
Azam kuwafunga raundi ya kwanza bao 1-0 huwa hawatabiriki, kwani Azam ikizembea
Stand inaweza kuwatoa nishai.
Kwa upande wa Mbeya City na Kagera Sugar
zimetofautiana kwa tofauti ya pointi tatu hivyo kila mmoja ni muhimu kushinda.
Kagera Sugar kama itashindwa kufanya vizuri
kuna hatari ya kushuka kwani timu tano zilizoko
nyuma yake ikiwemo hiyo ya Mbeya City zinafanana kwa pointi 28, kwa
maana kwamba zote zikifanya vizuri inaweza kujikuta ikiangukia nafasi ya 10.
Michezo mingine itakayopigwa kesho Jumapili ni
Mtibwa Sugar wakicheza dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Manungu na Tanzania
Prisons wakiwakaribisha Mgambo JKT kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Msimamo:
MP
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
+/-
|
Pts
|
|||||
1
|
23
|
16
|
4
|
3
|
47
|
14
|
33
|
52
|
||||
2
|
22
|
11
|
9
|
2
|
29
|
15
|
14
|
42
|
||||
3
|
23
|
10
|
8
|
5
|
31
|
17
|
14
|
38
|
||||
4
|
23
|
8
|
7
|
8
|
22
|
22
|
0
|
31
|
||||
5
|
24
|
7
|
8
|
9
|
16
|
26
|
-10
|
29
|
||||
6
|
23
|
6
|
10
|
7
|
22
|
23
|
-1
|
28
|
||||
7
|
23
|
6
|
10
|
7
|
19
|
21
|
-2
|
28
|
||||
8
|
23
|
7
|
7
|
9
|
21
|
27
|
-6
|
28
|
||||
9
|
23
|
8
|
4
|
11
|
18
|
25
|
-7
|
28
|
||||
10
|
24
|
6
|
10
|
8
|
16
|
23
|
-7
|
28
|
||||
11
|
23
|
6
|
7
|
10
|
17
|
23
|
-6
|
25
|
||||
12
|
24
|
5
|
10
|
9
|
15
|
22
|
-7
|
25
|
||||
13
|
23
|
6
|
7
|
10
|
18
|
26
|
-8
|
25
|
||||
14
|
23
|
3
|
13
|
7
|
15
|
22
|
-7
|
22
|
No comments:
Post a Comment