LONDON, England
KOCHA wa Liverpool Brendan Rodgers tayari anakabiliana na kibarua
kigumu kumshawishi nyota Raheem Sterling kusaijili mkataba mpya wa kuendelea
kuichezea timu hiyo.
Lakini gazeti la Starsport lilibainisha kuwa kocha huyo pia ana kazi
nyingine ya hatma ya Anfield kumshawishi kiungo Henderson naye kubaki katika
klabu hiyo.
Henderson ametupilia mbali mkataba mpya ambao ungekuwa na thamani
ya pauni 80,000 kwa wiki.
Mazungumzo zaidi yanafanywa lakini Chelsea wanafuatilia kwa makini
sana suala hilo.
Macho yanamfuatilia zaidi Sterling hasa baada ya mchezaji huyo
kupiga chini ofa ya Liverpool ya pauni Milioni 100,000 kwa wiki na kusimamisha
mazungumzo yote hadi mwisho wa msimu.
Lakini Sterling bado amebakisha miaka miwili katika mkataba wake
wasasa wakati makamu nahodha wa timu hiyo Henderson suala lake linaonekana ni
nyeti zaidi wakati mkataba wake umebaki mwaka mmoja tu.
Muingereza Henderson sasa ni mchezaji muhimu kwa Liverpool, ambapo
alinunuliwa na Liverpool kwa pauni Milioni 20 akitokea Sunderland mwaka 2011.
Matumaini ya Liverpool kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya yanazidi
kufifia baada ya timu hiyo kushindwa kuwemo katika nne bora, kufuatia kichapo
cha 4-1 Jumamosi dhidi ya Arsenal.
Na Rodgers anakiri kuwa, kutokuwemo katika Ligi ya Mabingwa huenda
kukatupa wakati mgumu kusajili katika kipindi cha majira ya joto.
"Nafikiri wachezaji wengi wanataka kucheza katika mashindano
makubwa na kama haupo katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya itakufanya wewe kuwa na
wakati mgumu, " alisema.
Alipoulizwa kama matumaini ya kufuzu kwa Ligi Kuu ya Mabingwa wa
Ulaya yamepotea, baada ya kufungwa na the Gunners na kufungwa nyumbani na Manchester
United, Rodgers alisema: "Nafikiri hivyo.
No comments:
Post a Comment