ISTANBUL, Uturuki
LIGI Kuu ya Uturuki imesimamishwa kwa wiki moja baada ya basi la
timu ya Fenerbahce kushambuliwa na kwa risasi Jumamosi.
Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF) lilitangaza uamuzi huo baada
ya mkutano na waziri wa michezo Jumatatu.
"Tunaamini tukio hile ni la kigaidi, ambalo liliwalenga sio
tu Fenerbahce bali pia wanamichezo wote wa michezo, ," alisema mwenyekiti
wa TFF Yildirim Demiroren.
"Tumeamua kuahirisha mechi zote za ligi kwa wiki moja."
Mabingwa watetezi Fenerbahce walikuwa wakisafiri kwenda uwanja wa
ndege wa Trabzon, kufuatia ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Rizespor, wakati
shambulizi hilo linatokea.
Derea wa basi hilo alikimbizwa hospitalini baada ya kujeruhiwa
kutokana na shambulizi hilo.
Katika taarifa yake katika mtandao wa TFF, Waziri wa Michezo Akif
Cagatay Kilic alisema dereva wa basi, aliyetambulika kama Ufuk Ki
ran, hali yake inaendelea vizuri.
Fenerbahce iliomba ligi hiyo iahirishwe ikisema: "tunafikiri
ni jambo lisilo kwepeka hadi hali hii ya kutisha itakapomalizika."
No comments:
Post a Comment