CAIRO, Misri
WAJUMBE wawili watachaguliwa kama wawakilishi wa bara la Afrika
katika Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la soka (CAF) Jumanne.
Shirikisho hilo la soka la Afrika linatakiwa kuchagua wawakilishi
wake watakaoingia katika jopo la watu wazito 25 wa bodi ya maamuzi ya FIFA.
Mtunisia Tarek Bouchamaoui na Constant Omari Selemani wa Kongo DRC
wanapewa nafasi kubwa ya kuongoza katika kura hizo.
Wawili hao wanaoonekana kumbwaga mjumbe kutoka Ivory Coast Jacques
Anouma kutoka katika kamati hiyo aliyoitumikia kwa takribani miaka nane.
Wajumbe kutoka nchi 54 pia wataombwa kuondoa kipengele cha sheria katika Katiba ya CAF kinachohusu
ukumo wa umri ili kuweza kumruhusu rais wa sasa wa shirikisho hilo Issa Hayatou
kuendelea kuongoza baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha sasa.
Kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Caf, iongozi waliofikia umri wa
miaka 70 wanatakiwa kuachia ngazi, hiyo wanataka kuondoa sheria hiyo ili watu
hao waruhusiwe kuendelea kuongoza.
Kitendo hicho kitafungua mlango kwa mzaliwa wa Cameroon- Hayatou, ambaye
kwa sasa ana umri wa miaka 68 na anayeongoza kwa muhula wa saba, kuendelea
kuongoza baada ya kumalizika kwa muda wake wasasa mwaka 2017.
Awali, Anouma alikuwa mpinzani mkubwa wa kinyang’anyiro cha nafasi hiyo ya uongozi
lakini sasa ameungana na Hayatou ambaye wapinzani wake wamepungua nguvu
kutokana na siasa za soka.
Rais wa Chama cha Soka cha Algeria Mohamed Raouraoua, ambaye awali
alionesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya CAF, aliondoa jina lake
katika uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment